kwa sababu wametenda yaliyo mabaya machoni pangu, na kunikasirisha, tangu siku ile walipotoka baba zao katika Misri, hata leo hivi.
Maombolezo 1:5 - Swahili Revised Union Version Watesi wake wamekuwa kichwa, Adui zake hufanikiwa; Kwa kuwa BWANA amemtesa Kwa sababu ya wingi wa makosa yake; Watoto wake wadogo wamechukuliwa mateka Mbele yake huyo mtesi. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Adui zake ndio wanaoutawala na wanafanikiwa, kwani Mwenyezi-Mungu ameutesa kwa sababu ya makosa mengi. Watoto wake wametekwa na kupelekwa mbali. Biblia Habari Njema - BHND Adui zake ndio wanaoutawala na wanafanikiwa, kwani Mwenyezi-Mungu ameutesa kwa sababu ya makosa mengi. Watoto wake wametekwa na kupelekwa mbali. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Adui zake ndio wanaoutawala na wanafanikiwa, kwani Mwenyezi-Mungu ameutesa kwa sababu ya makosa mengi. Watoto wake wametekwa na kupelekwa mbali. Neno: Bibilia Takatifu Adui zake wamekuwa mabwana zake, watesi wake wana amani. Mwenyezi Mungu amemletea huzuni kwa sababu ya dhambi zake nyingi. Watoto wake wameenda uhamishoni, wamekuwa mateka mbele ya adui. Neno: Maandiko Matakatifu Adui zake wamekuwa mabwana zake, watesi wake wana raha. bwana amemletea huzuni kwa sababu ya dhambi zake nyingi. Watoto wake wamekwenda uhamishoni, mateka mbele ya adui. BIBLIA KISWAHILI Watesi wake wamekuwa kichwa, Adui zake hufanikiwa; Kwa kuwa BWANA amemtesa Kwa sababu ya wingi wa makosa yake; Watoto wake wadogo wamechukuliwa mateka Mbele yake huyo mtesi. |
kwa sababu wametenda yaliyo mabaya machoni pangu, na kunikasirisha, tangu siku ile walipotoka baba zao katika Misri, hata leo hivi.
Kwa maana siku ya kutaabika, siku ya kukanyagwa, siku ya fujo inakuja, itokayo kwa Bwana, BWANA wa majeshi, katika bonde la Maono; inabomoa kuta; na kuililia milima.
Watu wako watakatifu waliumiliki kwa kitambo tu; adui zetu wamepakanyaga patakatifu pako.
Hema yangu imetekwa nyara, kamba zangu zote zimekatika; watoto wangu wameniacha na kwenda zao, pia hawako. Hakuna mtu atakayenitandikia tena hema yangu, na kuyatundika mapazia yangu.
Nimeiacha nyumba yangu, nimeutupa urithi wangu; nimemtia mpenzi wangu katika mikono ya adui zake.
Katika manabii wa Yerusalemu nimeona neno linalochukiza sana; hufanya zinaa; huenda katika maneno ya uongo, hutia nguvu mikono ya watendao maovu, hata ikawa hapana mtu arejeaye na kuuacha uovu wake; wote pia wamekuwa kama Sodoma kwangu, na wenyeji wake kama Gomora.
Basi, Nebuzaradani, mkuu wa askari walinzi, akawachukua mateka mabaki ya watu waliosalia katika mji mpaka Babeli, na hao pia waliouacha mji na kujiunga naye, na mabaki ya watu waliosalia.
Je! Nisiwapatilize kwa mambo hayo? Asema BWANA; na nafsi yangu, je! Nisijilipizie kisasi juu ya taifa la namna hii?
Mimi ninayalilia mambo hayo; Jicho langu, jicho langu linachuruzika machozi; Kwa kuwa mfariji yuko mbali nami, Ambaye ilimpasa kunihuisha nafsi; Watoto wangu wameachwa peke yao, Kwa sababu huyo adui ameshinda.
BWANA ndiye mwenye haki; Maana nimeiasi amri yake; Sikieni, nawasihi, enyi watu wote, Mkayatazame majonzi yangu; Wasichana wangu na wavulana wangu Wamechukuliwa mateka.
Yerusalemu amefanya dhambi sana; Kwa hiyo amekuwa kama kitu kichafu; Wote waliomheshimu wanamdharau, Kwa sababu wameuona uchi wake; Naam, yeye anaugua, Na kujigeuza aende nyuma.
BWANA ameyatenda aliyoyakusudia; amelitimiza neno lake, Aliloliamuru siku za kale; Ameangusha hata chini, Wala hakuona huruma; Naye amemfurahisha adui juu yako, Ameitukuza pembe ya watesi wako.
Nami, jicho langu halitaachilia, wala sitakuwa na huruma; lakini nitaleta njia yao juu ya vichwa vyao.
Ndipo akaniambia, Uovu wa nyumba ya Israeli na Yuda ni mwingi sana, nayo nchi imejaa damu, nao mji umejaa kupotosha hukumu; maana husema, BWANA ameiacha nchi hii, naye BWANA haoni.
Kwa sababu najua baada ya kufa kwangu mtajiharibu kabisa, na kukengeuka katika njia niliyowaamuru; nayo mabaya yatawapata siku za mwisho, kwa vile mtakavyofanya maovu machoni pa BWANA kumtia kasirani kwa kazi ya mikono yenu.