Na tazama, mwanamke Mkanaani wa mipaka ile akatokea, akampazia sauti akisema, Unirehemu, Bwana, Mwana wa Daudi; binti yangu amepagawa sana na pepo.
Luka 6:18 - Swahili Revised Union Version na wale waliosumbuliwa na pepo wachafu; waliponywa. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Aliwaponya pia wote waliokuwa wanasumbuliwa na pepo wachafu. Biblia Habari Njema - BHND Aliwaponya pia wote waliokuwa wanasumbuliwa na pepo wachafu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Aliwaponya pia wote waliokuwa wanasumbuliwa na pepo wachafu. Neno: Bibilia Takatifu Walikuwa wamekuja kumsikiliza na kuponywa magonjwa yao. Wale waliokuwa wakiteswa na pepo wachafu akawaponya. Neno: Maandiko Matakatifu Walikuwa wamekuja kumsikiliza na kuponywa magonjwa yao. Wale waliokuwa wakiteswa na pepo wachafu akawaponya. BIBLIA KISWAHILI na wale waliosumbuliwa na pepo wachafu; waliponywa. |
Na tazama, mwanamke Mkanaani wa mipaka ile akatokea, akampazia sauti akisema, Unirehemu, Bwana, Mwana wa Daudi; binti yangu amepagawa sana na pepo.
Bwana, umrehemu mwanangu, kwa kuwa ana kifafa, na kuteswa vibaya; maana mara nyingi huanguka motoni, na mara nyingi majini.
Akashuka pamoja nao, akasimama mahali tambarare, pamoja na wanafunzi wake wengi, na makutano makubwa ya watu waliotoka Yudea wote na Yerusalemu, na pwani ya Tiro na Sidoni; waliokuja kumsikiliza na kuponywa magonjwa yao;
Na makutano yote walikuwa wakitaka kumgusa, kwa sababu uweza ulikuwa ukimtoka ukiwaponya wote.
Nayo makundi ya watu wa miji iliyoko kandokando ya Yerusalemu wakakutanika, wakileta wagonjwa, nao walioudhiwa na pepo wachafu; nao wote wakaponywa.