Luka 4:7 - Swahili Revised Union Version Basi, wewe ukisujudu mbele yangu yote yatakuwa yako. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Hivi vyote vitakuwa mali yako wewe, kama ukiniabudu.” Biblia Habari Njema - BHND Hivi vyote vitakuwa mali yako wewe, kama ukiniabudu.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Hivi vyote vitakuwa mali yako wewe, kama ukiniabudu.” Neno: Bibilia Takatifu Hivyo ukinisujudia na kuniabudu, vyote vitakuwa vyako.” Neno: Maandiko Matakatifu Hivyo ikiwa utanisujudia na kuniabudu, vyote vitakuwa vyako.” BIBLIA KISWAHILI Basi, wewe ukisujudu mbele yangu yote yatakuwa yako. |
BWANA asema hivi, Kazi ya Misri, na bidhaa ya Kushi, na Waseba, watu walio warefu, watakujia, nao watakuwa wako; watakufuata; watakuja katika minyororo; wataanguka chini mbele yako, watakuomba, wakisema, Hakika Mungu yu ndani yako; wala hapana mwingine, hapana Mungu tena.
Watu wamwagao dhahabu kutoka mfukoni, na kupima fedha katika mizani, huajiri mfua dhahabu, akaifanya mungu; huanguka, naam, huabudu.
Wakaingia nyumbani, wakamwona mtoto pamoja na Mariamu mamaye, wakaanguka wakamsujudia; nao walipokwisha kufungua hazina zao, wakamtolea tunu; dhahabu, uvumba na manemane.
Ibilisi akamwambia, Nitakupa wewe enzi hii yote, na fahari yake, kwa kuwa imo mikononi mwangu, nami humpa yeyote kama nipendavyo.
Yesu akajibu akamwambia, Imeandikwa, Msujudie Bwana Mungu wako, umwabudu yeye peke yake.
Alipomwona Yesu alipiga kelele, akaanguka mbele yake, akasema kwa sauti kuu, Nina nini nawe, Yesu, Mwana wa Mungu Aliye Juu? Nakusihi usinitese.
Nami Yohana ndimi niliyeyasikia na kuyaona mambo hayo. Na hapo nilipoyasikia na kuyaona nilianguka, ili nisujudu mbele ya miguu ya malaika yule mwenye kunionesha hayo.
ndipo hao wazee ishirini na wanne huanguka mbele zake yeye aketiye juu ya kile kiti cha enzi, nao humsujudia yeye aliye hai hata milele na milele, nao hutupa taji zao mbele ya kile kiti cha enzi, wakisema,
Hata alipokitwaa kile kitabu, hao wenye uhai wanne na wale wazee ishirini na wanne wakaanguka mbele za Mwana-kondoo, kila mmoja wao ana kinubi, na vitasa vya dhahabu vilivyojaa manukato, ambayo ni maombi ya watakatifu.