Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona.
Luka 23:16 - Swahili Revised Union Version Kwa hiyo nitamrudi, kisha nitamfungua. [ Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Hivyo, nitaamuru apigwe viboko, halafu nitamwachilia.” [ Biblia Habari Njema - BHND Hivyo, nitaamuru apigwe viboko, halafu nitamwachilia.” [ Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Hivyo, nitaamuru apigwe viboko, halafu nitamwachilia.” Neno: Bibilia Takatifu Kwa hiyo nitaamuru apigwe mijeledi na kumwachilia.” [ Neno: Maandiko Matakatifu Kwa hiyo nitaamuru apigwe mijeledi na kumwachia.” [ BIBLIA KISWAHILI Kwa hiyo nitamrudi, kisha nitamfungua. [ |
Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona.
Pilato kwa kupenda kuwaridhisha watu, akawafungulia Baraba; akamtoa Yesu, baada ya kumpiga mijeledi, ili asulubiwe.
Akawaambia mara ya tatu, Kwa sababu gani? Huyu ametenda uovu gani? Sikuona kwake hata neno lipasalo kufa. Basi nikiisha kumrudi nitamfungua.
Msihukumu, nanyi hamtahukumiwa; msilaumu, nanyi hamtalaumiwa; sameheni, nanyi mtasamehewa.
Paulo akawaambia, Wametupiga mbele ya watu wote bila kutuhukumu, na sisi tu Warumi, tena wametutupa gerezani; na sasa wanataka kututoa kwa siri? Sivyo, lakini na waje wenyewe wakatutoe.