akazichukua hazina za nyumba ya BWANA, na hazina za nyumba ya mfalme; akazichukua zote. Akazichukua pia ngao zote za dhahabu alizozifanya Sulemani.
Luka 21:1 - Swahili Revised Union Version Akainua macho yake akawaona matajiri wakitia sadaka zao katika sanduku la hazina. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Yesu alitazama kwa makini, akawaona matajiri walivyokuwa wanatia sadaka zao katika hazina ya hekalu, Biblia Habari Njema - BHND Yesu alitazama kwa makini, akawaona matajiri walivyokuwa wanatia sadaka zao katika hazina ya hekalu, Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Yesu alitazama kwa makini, akawaona matajiri walivyokuwa wanatia sadaka zao katika hazina ya hekalu, Neno: Bibilia Takatifu Isa alipoinua macho yake, aliwaona matajiri wakiweka sadaka zao kwenye sanduku la hazina ya Hekalu. Neno: Maandiko Matakatifu Isa alipoinua macho yake, aliwaona matajiri wakiweka sadaka zao kwenye sanduku la hazina ya Hekalu. BIBLIA KISWAHILI Akainua macho yake akawaona matajiri wakitia sadaka zao katika sanduku la hazina. |
akazichukua hazina za nyumba ya BWANA, na hazina za nyumba ya mfalme; akazichukua zote. Akazichukua pia ngao zote za dhahabu alizozifanya Sulemani.
Lakini Yehoyada kuhani akatwaa kasha, akatoboa tundu katika kifuniko chake, akaliweka karibu na madhabahu, upande wa kulia mtu aingiapo nyumbani mwa BWANA; na makuhani, waliolinda mlangoni, wakatia ndani yake fedha yote iliyoletwa nyumbani mwa BWANA.
Akatoa huko hazina zote za nyumba ya BWANA, na hazina za nyumba ya mfalme, akavikatakata vyombo vyote vya dhahabu ambavyo Sulemani, mfalme wa Israeli, alivitengeneza katika hekalu la BWANA, kama BWANA alivyosema.
Na vyombo vyote vya nyumba ya Mungu, vikubwa kwa vidogo, na hazina za nyumba ya BWANA, na hazina za mfalme, na za wakuu wake; vyote pia akavileta Babeli.
Nami nikawaweka watunza hazina juu ya hazina, yaani, Shelemia kuhani, na Sadoki mwandishi, na wa Walawi, Pedaya; na wa pili wao alikuwa Hanani, mwana wa Zakuri, mwana wa Matania; kwani walihesabiwa kuwa waaminifu, na ilikuwa juu yao kuwagawia ndugu zao.
Wakuu wa makuhani wakavitwaa vile vipande vya fedha, wakasema, Si halali kuviweka katika sanduku ya sadaka, kwa kuwa ni fedha ya damu.
Wanakula nyumba za wajane, na kwa unafiki husali sala ndefu. Hao watapata hukumu iliyo kuu.
Maneno hayo aliyasema alipokuwa akifundisha hekaluni, katika chumba cha hazina; wala hakuna mtu aliyemkamata, kwa sababu saa yake ilikuwa haijafika bado.
Lakini fedha yote, na dhahabu, na vyombo vya shaba, na chuma, ni vitakatifu kwa BWANA; vitaletwa katika hazina ya BWANA.
Kisha wakauteketeza mji kwa moto, na vitu vyote vilivyokuwa ndani yake; bali fedha, na dhahabu, na vyombo vya shaba, na vya chuma, wakavitia katika hazina ya nyumba ya BWANA.