Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yoshua 6:19 - Swahili Revised Union Version

19 Lakini fedha yote, na dhahabu, na vyombo vya shaba, na chuma, ni vitakatifu kwa BWANA; vitaletwa katika hazina ya BWANA.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

19 Lakini fedha yote, dhahabu, vyombo vya shaba na chuma ni vitakatifu kwa Mwenyezi-Mungu; hivyo vitawekwa katika hazina ya Mwenyezi-Mungu.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

19 Lakini fedha yote, dhahabu, vyombo vya shaba na chuma ni vitakatifu kwa Mwenyezi-Mungu; hivyo vitawekwa katika hazina ya Mwenyezi-Mungu.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

19 Lakini fedha yote, dhahabu, vyombo vya shaba na chuma ni vitakatifu kwa Mwenyezi-Mungu; hivyo vitawekwa katika hazina ya Mwenyezi-Mungu.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

19 Fedha yote na dhahabu, vyombo vya shaba na chuma ni vitakatifu kwa Mwenyezi Mungu, lazima viletwe katika hazina yake.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

19 Fedha yote na dhahabu, vyombo vya shaba na chuma ni vitakatifu kwa bwana, lazima viletwe katika hazina yake.”

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

19 Lakini fedha yote, na dhahabu, na vyombo vya shaba, na chuma, ni vitakatifu kwa BWANA; vitaletwa katika hazina ya BWANA.

Tazama sura Nakili




Yoshua 6:19
25 Marejeleo ya Msalaba  

hivi pia mfalme Daudi akavifanya wakfu kwa BWANA, pamoja na hiyo fedha, na dhahabu alizofanya wakfu za mataifa yote aliowashinda;


akazichukua hazina za nyumba ya BWANA, na hazina za nyumba ya mfalme; akazichukua zote. Akazichukua pia ngao zote za dhahabu alizozifanya Sulemani.


Hivyo kazi yote aliyoifanya mfalme Sulemani katika nyumba ya BWANA ikamalizika. Sulemani akaviingiza vile vitu alivyovitakasa Daudi baba yake, yaani, fedha, na dhahabu, na vyombo; akavitia ndani ya hazina za nyumba ya BWANA.


Akatoa huko hazina zote za nyumba ya BWANA, na hazina za nyumba ya mfalme, akavikatakata vyombo vyote vya dhahabu ambavyo Sulemani, mfalme wa Israeli, alivitengeneza katika hekalu la BWANA, kama BWANA alivyosema.


Hivi pia mfalme Daudi akavifanya wakfu kwa BWANA, pamoja na hiyo fedha na dhahabu, aliyoteka nyara kwa mataifa yote; kwa Edomu, na kwa Moabu, na kwa wana wa Amoni, na kwa Wafilisti, na kwa Amaleki.


Na katika Walawi; Ahia mtunzaji wa hazina ya nyumba ya Mungu, pamoja na hazina ya vitu vilivyowekwa wakfu.


Huyo Shelomothi na ndugu zake walikuwa wasimamizi wa hazina zote za vitu vilivyowekwa wakfu, alivyoviweka wakfu mfalme Daudi, na hao wakuu wa koo za mababa, na maofisa wa maelfu na wa mamia, na makamanda wa jeshi.


Katika nyara zilizopatikana vitani, waliweka wakfu sehemu, ili kuitengeneza nyumba ya BWANA.


Na vyote alivyoviweka wakfu Samweli mwonaji, na Sauli mwana wa Kishi, na Abneri mwana wa Neri, na Yoabu mwana wa Seruya; na mtu yeyote aliyekiweka wakfu kitu chochote, kilikuwa chini ya mkono wa Shelomothi na nduguze.


na mfano wa yote aliyokuwa nao rohoni, kuhusu nyua za nyumba ya BWANA, na ya vyumba vyote vilivyoizunguka, ya hazina za nyumba ya Mungu, na ya hazina za vitu vilivyowekwa wakfu;


Akavileta nyumbani mwa Mungu vitu alivyovitakasa babaye, na vile alivyovitakasa mwenyewe, fedha, na dhahabu, na vyombo.


Wakayaingiza matoleo na zaka na vitu vilivyowekwa wakfu, kwa uaminifu; Konania, Mlawi aliwekwa kuwa mkuu na Shimei nduguye akawa masaidizi wake.


Naye kuhani, mwana wa Haruni, atakuwako pamoja na Walawi, watwaapo zaka Walawi; nao Walawi wataipandisha zaka ya hizo zaka nyumbani kwa Mungu wetu, vyumbani, katika nyumba ya hazina.


Basi Ebedmeleki akawachukua watu hao pamoja naye, akaingia ndani ya nyumba ya mfalme chini ya ghala, akatoa mle nguo zilizotupwa, na vitambaa vikuukuu, akamteremshia Yeremia shimoni kwa kamba.


Lakini mwaka wa nne matunda yake yote yatakuwa ni matakatifu, kwa ajili ya kumpa BWANA shukrani.


Haya, simama upure, Ee binti Sayuni; kwa maana nitafanya pembe yako kuwa chuma, na kwato zako kuwa shaba; nawe utapondaponda mataifa mengi, na faida yao utaiweka wakfu kwa BWANA, na mali zao kwa BWANA wa dunia yote.


Nao wakatwaa hizo nyara zote, na mateka yote, ya wanadamu na ya wanyama.


Nao wakawaleta mateka ya wanadamu, na mateka ya wanyama, na hizo nyara, na kuyaweka mbele ya Musa, na mbele ya Eleazari kuhani, na mbele ya mkutano wa wana wa Israeli, hapo kambini katika nchi tambarare za Moabu, zilizo karibu na Yordani hapo Yeriko.


lakini dhahabu, na fedha, na shaba, na chuma, na bati, na risasi,


Wakuu wa makuhani wakavitwaa vile vipande vya fedha, wakasema, Si halali kuviweka katika sanduku ya sadaka, kwa kuwa ni fedha ya damu.


Naye akaketi kulielekea sanduku la hazina, akatazama jinsi mkutano watiavyo mapesa katika sanduku. Matajiri wengi wakatia mengi.


Israeli wamefanya dhambi, naam, wamelivunja agano langu nililowaagiza; naam, wametwaa baadhi ya vitu vilivyowekwa wakfu; tena wameiba, tena wameficha na kuvitia pamoja na vitu vyao wenyewe.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo