BWANA, mkono wako umeinuliwa, lakini hawaoni; lakini watauona wivu wako kwa ajili ya watu wako, nao watatahayari; naam, moto utawala adui zako.
Luka 20:7 - Swahili Revised Union Version Wakajibu, kwamba, Hatujui ulikotoka. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Basi, wakamwambia, “Hatujui mamlaka hayo yalitoka wapi.” Biblia Habari Njema - BHND Basi, wakamwambia, “Hatujui mamlaka hayo yalitoka wapi.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Basi, wakamwambia, “Hatujui mamlaka hayo yalitoka wapi.” Neno: Bibilia Takatifu Basi wakajibu, “Hatujui ulikotoka.” Neno: Maandiko Matakatifu Basi wakajibu, “Hatujui ulikotoka.” BIBLIA KISWAHILI Wakajibu, kwamba, Hatujui ulikotoka. |
BWANA, mkono wako umeinuliwa, lakini hawaoni; lakini watauona wivu wako kwa ajili ya watu wako, nao watatahayari; naam, moto utawala adui zako.
kwa sababu hiyo mimi nitafanya tena kazi ya ajabu kati ya watu hawa, kazi ya ajabu na mwujiza; na akili za watu wao wenye akili zitapotea, na ufahamu wa wenye busara wao utafichwa.
Na nitazamapo, hapana mtu, hata katika watu hao hapana mshauri mmoja, ambaye, nikimwuliza, aweza kunijibu neno.
Hawajui wala hawafikiri; maana amewafumba macho, wasione, na mioyo yao, wasiweze kufahamu.
Ole wake mchungaji asiyefaa, aliachaye kundi! Upanga utakuwa juu ya mkono wake, na juu ya jicho lake la kulia; mkono wake utakuwa umekauka kabisa, na jicho lake la kulia litakuwa limepofuka.
Na tukisema ulitoka kwa wanadamu, watu wote watatupiga kwa mawe, kwa kuwa wamemkubali Yohana kuwa ni nabii.
Yesu akasema, Mimi nimekuja ulimwenguni humu kwa hukumu, ili wao wasioona waone, nao wanaoona wawe vipofu.
Mkijua kwanza neno hili ya kwamba katika siku za mwisho watakuja na dhihaka zao watu wenye kudhihaki, wafuatao tamaa zao wenyewe,