Biblia ya mtandaoni

Matangazo


Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya




Luka 20:22 - Swahili Revised Union Version

Je! Ni halali tumpe Kaisari kodi, au sivyo?

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Basi, tuambie kama ni halali au la, kulipa kodi kwa Kaisari!”

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Basi, tuambie kama ni halali au la, kulipa kodi kwa Kaisari!”

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Basi, tuambie kama ni halali au la, kulipa kodi kwa Kaisari!”

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Je, ni halali sisi kulipa kodi kwa Kaisari, au la?”

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Je, ni halali sisi kulipa kodi kwa Kaisari, au la?”

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Je! Ni halali tumpe Kaisari kodi, au sivyo?

Tazama sura
Tafsiri zingine



Luka 20:22
14 Marejeleo ya Msalaba  

Basi, ijulikane kwa mfalme, ya kuwa mji huu ukijengwa, na kuta zake zikimalizika, hawatatoa kodi, wala ada, wala ushuru, na mwisho wake wafalme watapata hasara.


Tangu siku za baba zetu tumekuwa na hatia kupita kiasi hadi leo; na kwa sababu ya maovu yetu sisi, na wafalme wetu, na makuhani wetu, tumetiwa katika mikono ya wafalme wa nchi hizi, tumepigwa kwa upanga, tumechukuliwa mateka, tumenyang'anywa mali zetu, tumetiwa haya nyuso zetu, kama hivi leo.


Tena walikuwako wengine waliosema, Tumekopa fedha ili kulipa kodi ya mfalme kwa kuweka rehani mashamba yetu, na mizabibu yetu.


Nayo yawapatia faida nyingi wafalme uliowaweka kututawala kwa sababu ya dhambi zetu; tena wana mamlaka juu ya miili yetu, na juu ya wanyama wetu, kadiri wapendavyo, nasi tuko katika dhiki kuu.


Naye alipoingia nyumbani, Yesu alitangulia kumwuliza, akisema, Waonaje, Simoni? Wafalme wa dunia hutwaa kodi ama ushuru kwa watu gani? Kwa wana wao au kwa wageni?


Wakamwuliza, wakisema, Mwalimu, twajua ya kwamba wasema na kufundisha yaliyo ya haki, wala hujali cheo cha mtu, bali unafundisha njia ya Mungu kwa kweli.


Lakini yeye alitambua hila yao, akawaambia,


Wakaanza kumshitaki, wakisema, Tumemwona huyu akipotosha taifa letu, na kuwazuia watu wasimpe Kaisari kodi, akisema kwamba yeye mwenyewe ni Kristo, mfalme.


Baada ya mtu huyo aliondoka Yuda Mgalilaya, siku zile za kuandikiwa orodha, akawavuta watu kadhaa nyuma yake, naye pia akapotea na wote waliomsadiki wakatawanyika.


Wapeni wote haki zao; mtu wa kodi, kodi; mtu wa ushuru, ushuru; astahiliye hofu, hofu; astahiliye heshima, heshima.


usiache kumweka yule atakayechaguliwa na BWANA, Mungu wako, awe mfalme juu yako; umweke mmoja katika ndugu zako awe mfalme juu yako; usimtawaze mgeni juu yako, ambaye si ndugu yako.