Luka 2:32 - Swahili Revised Union Version Nuru ya kuwa mwangaza wa Mataifa, Na kuwa utukufu wa watu wako Israeli. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mwanga utakaowaangazia watu wa mataifa, na utukufu kwa watu wako Israeli.” Biblia Habari Njema - BHND Mwanga utakaowaangazia watu wa mataifa, na utukufu kwa watu wako Israeli.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mwanga utakaowaangazia watu wa mataifa, na utukufu kwa watu wako Israeli.” Neno: Bibilia Takatifu nuru kwa ajili ya ufunuo kwa watu wa Mataifa na kwa ajili ya utukufu kwa watu wako Israeli.” Neno: Maandiko Matakatifu nuru kwa ajili ya ufunuo kwa watu wa Mataifa na kwa ajili ya utukufu kwa watu wako Israeli.” BIBLIA KISWAHILI Nuru ya kuwa mwangaza wa Mataifa, Na kuwa utukufu wa watu wako Israeli. |
Na itakuwa katika siku hiyo, shina la Yese lisimamalo kuwa ishara kwa makabila ya watu, yeye ndiye ambaye mataifa watamtafuta; na mahali pake pa kupumzikia patakuwa na utukufu.
Siku hiyo chipukizi la BWANA litakuwa zuri, lenye utukufu, na matunda ya nchi yatakuwa mema sana, na kupendeza, kwa ajili ya Waisraeli wale waliookoka.
naam, asema hivi, Ni neno dogo sana wewe kuwa mtumishi wangu ili kuyainua makabila ya Yakobo, na kuwarejesha watu wa Israeli waliohifadhiwa; zaidi ya hayo nitakutoa uwe nuru ya mataifa, upate kuwa wokovu wangu hata miisho ya dunia.
kuwaambia waliofungwa, Haya, tokeni; na hao walio katika giza, Jionesheni. Watajilisha katika njia, na juu ya majabali watapata malisho.
Nisikilizeni mimi, enyi watu wangu; nisikieni, taifa langu; maana sheria itatoka kwangu, na kutoa haki yangu iwe nuru ya mataifa.
Jua halitakuwa nuru yako tena wakati wa mchana, Wala mwezi hautakupa nuru kwa mwangaza wake; Bali BWANA atakuwa nuru ya milele kwako, Na Mungu wako atakuwa utukufu wako.
Watu wale waliokwenda katika giza Wameona nuru kuu; Wale waliokaa katika nchi ya uvuli wa mauti, Nuru imewaangaza.
Je! Taifa wamebadili miungu yao, ingawa siyo miungu? Lakini watu wangu wameubadili utukufu wao kwa ajili ya kitu kisichofaidia.
Kwa maana mimi, asema BWANA, nitakuwa ukuta wa moto kuuzunguka pande zote, nami nitakuwa huo utukufu ndani yake.
Watu wale waliokaa katika giza Wameona mwanga mkuu, Nao waliokaa katika nchi na uvuli wa mauti Mwanga umewazukia.
Malaika akawaambia, Msiogope; kwa kuwa mimi ninawaletea habari njema ya furaha kuu itakayokuwa kwa watu wote;
ya kwamba Kristo hana budi kuteswa na ya kwamba yeye kwanza kwa kufufuliwa katika wafu atatangaza habari za nuru kwa watu wake na kwa watu wa Mataifa.
Basi ijulikane kwenu ya kwamba wokovu huu wa Mungu umepelekwa kwa Mataifa, nao watasikia! [
Na mji ule hauhitaji jua wala mwezi kuuangaza, kwa maana utukufu wa Mungu huutia nuru, na taa yake ni Mwana-kondoo.