Nitakasie mimi wazaliwa wa kwanza wote, kila afunguaye tumbo katika wana wa Israeli, wa binadamu na wa mnyama; ni wangu huyo.
Luka 2:23 - Swahili Revised Union Version (kama ilivyoandikwa katika sheria ya Bwana, Kila mtoto wa kiume aliye kifungua mimba wa mamaye na aitwe mtakatifu kwa Bwana), Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Katika sheria ya Bwana imeandikwa: “Kila mzaliwa wa kwanza wa kiume atawekwa wakfu kwa Bwana.” Biblia Habari Njema - BHND Katika sheria ya Bwana imeandikwa: “Kila mzaliwa wa kwanza wa kiume atawekwa wakfu kwa Bwana.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Katika sheria ya Bwana imeandikwa: “Kila mzaliwa wa kwanza wa kiume atawekwa wakfu kwa Bwana.” Neno: Bibilia Takatifu (kama ilivyoandikwa katika Torati ya Mwenyezi Mungu, kwamba, “Kila mtoto wa kiume kifungua mimba atawekwa wakfu kwa Mwenyezi Mungu”), Neno: Maandiko Matakatifu (kama ilivyoandikwa katika Torati ya Bwana Mwenyezi, kwamba, “Kila mtoto wa kiume kifungua mimba atawekwa wakfu kwa Bwana Mwenyezi Mungu”), BIBLIA KISWAHILI (kama ilivyoandikwa katika sheria ya Bwana, Kila mtoto wa kiume aliye kifungua mimba wa mamaye na aitwe mtakatifu kwa Bwana), |
Nitakasie mimi wazaliwa wa kwanza wote, kila afunguaye tumbo katika wana wa Israeli, wa binadamu na wa mnyama; ni wangu huyo.
Usikawie kuleta malimbuko ya matunda yako na ya vinywaji vyako. Mzaliwa wa kwanza katika wanao wanaume utanipa mimi.
Kila kifunguacho mimba ni changu mimi; na wanyama wako wote walio wa kiume, wazaliwa wa kwanza wa ng'ombe na wa kondoo.
Kila kifunguacho tumbo, cha wenye mwili wote watakachomsogezea BWANA cha wanadamu na cha wanyama, ni chako; lakini mzaliwa wa kwanza wa binadamu, huna budi utamkomboa, na mzaliwa wa kwanza wa wanyama wasio safi utamkomboa.
kwa kuwa hao wazaliwa wa kwanza wote ni wangu; katika siku ile niliyowapiga wazaliwa wa kwanza wote katika nchi ya Misri nikajiwekea wakfu wazaliwa wa kwanza wote wa Israeli, wa wanadamu na wa wanyama; watakuwa wangu; mimi ndimi BWANA.