Luka 2:19 - Swahili Revised Union Version Lakini Mariamu akayaweka maneno hayo yote, akiyafikiri moyoni mwake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Lakini Maria aliyaweka na kuyatafakari mambo hayo yote moyoni mwake. Biblia Habari Njema - BHND Lakini Maria aliyaweka na kuyatafakari mambo hayo yote moyoni mwake. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Lakini Maria aliyaweka na kuyatafakari mambo hayo yote moyoni mwake. Neno: Bibilia Takatifu Lakini Mariamu akayaweka mambo haya yote moyoni mwake na kuyatafakari. Neno: Maandiko Matakatifu Lakini Mariamu akayaweka mambo haya yote moyoni mwake na kuyatafakari. BIBLIA KISWAHILI Lakini Mariamu akayaweka maneno hayo yote, akiyafikiri moyoni mwake. |
Naye akanifundisha, akaniambia, Moyo wako uyahifadhi maneno yangu; Shika amri zangu ukaishi.
Huu ndio mwisho wa jambo lile. Nami, Danieli, fikira zangu zilinifadhaisha, na uso wangu ulinibadilika; lakini nililiweka jambo hilo moyoni mwangu.
Ni nani aliye na hekima, naye atayafahamu mambo haya? Ni nani aliye na busara, naye atayajua? Kwa maana njia za BWANA zimenyoka, nao wenye haki watakwenda katika njia hizo; bali waasio wataanguka ndani yake.
Na wote walioyasikia wakayaweka mioyoni mwao, wakisema, Mtoto huyu atakuwa wa namna gani? Kwa sababu mkono wa Bwana ulikuwa pamoja naye.
Akashuka pamoja nao mpaka Nazareti, naye alikuwa akiwatii; na mamaye aliyaweka hayo yote moyoni mwake.