Wewe wamlaki yeye afurahiaye yaliyo haki na kuyatenda, watu wale wakukumbukao katika njia zako; tazama, ulikuwa na hasira, nasi tulitenda dhambi; tumekuwa katika dhambi kwa muda mrefu, nasi Je! Tutaokolewa?
Luka 19:6 - Swahili Revised Union Version Akafanya haraka, akashuka, akamkaribisha kwa furaha. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Zakayo akashuka haraka, akamkaribisha kwa furaha. Biblia Habari Njema - BHND Zakayo akashuka haraka, akamkaribisha kwa furaha. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Zakayo akashuka haraka, akamkaribisha kwa furaha. Neno: Bibilia Takatifu Hivyo Zakayo akashuka upesi, akamkaribisha Isa nyumbani mwake kwa furaha kubwa. Neno: Maandiko Matakatifu Hivyo Zakayo akashuka upesi, akamkaribisha Isa nyumbani kwake kwa furaha kubwa. BIBLIA KISWAHILI Akafanya haraka, akashuka, akamkaribisha kwa furaha. |
Wewe wamlaki yeye afurahiaye yaliyo haki na kuyatenda, watu wale wakukumbukao katika njia zako; tazama, ulikuwa na hasira, nasi tulitenda dhambi; tumekuwa katika dhambi kwa muda mrefu, nasi Je! Tutaokolewa?
Na Yesu, alipofika mahali pale, alitazama juu, akamwambia, Zakayo, shuka upesi, kwa kuwa leo imenipasa kushinda nyumbani mwako.
Hata watu walipoona, walinung'unika wote, wakisema, Ameingia kukaa kwa mtu mwenye dhambi.
Na Lawi akamfanyia karamu kubwa nyumbani mwake; palikuwa na mkutano mkuu wa watoza ushuru na watu wengineo waliokuwa wameketi chakulani pamoja nao.
Hata alipokwisha kubatizwa, yeye na nyumba yake, akatusihi, akisema, Kama mmeniona kuwa mwaminifu kwa Bwana, ingieni nyumbani mwangu mkakae. Akatusihi sana.
Akawaleta juu nyumbani kwake, akawaandalia chakula, akafurahi sana, yeye na nyumba yake yote, maana amekwisha kumwamini Mungu.
Nao waliolipokea neno lake wakabatizwa; na siku ile wakaongezeka watu wapatao elfu tatu.