nami nitawabariki wakubarikio, naye akulaaniye nitamlaani; na katika wewe jamaa zote za dunia watabarikiwa.
Luka 1:55 - Swahili Revised Union Version Kama alivyowaambia baba zetu, Abrahamu na uzao wake hata milele. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema kama alivyowaahidia wazee wetu, Abrahamu na wazawa wake hata milele.” Biblia Habari Njema - BHND kama alivyowaahidia wazee wetu, Abrahamu na wazawa wake hata milele.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza kama alivyowaahidia wazee wetu, Abrahamu na wazawa wake hata milele.” Neno: Bibilia Takatifu Ibrahimu na uzao wake milele, kama alivyowaahidi baba zetu.” Neno: Maandiko Matakatifu Ibrahimu na uzao wake milele, kama alivyowaahidi baba zetu.” BIBLIA KISWAHILI Kama alivyowaambia baba zetu, Abrahamu na uzao wake hata milele. |
nami nitawabariki wakubarikio, naye akulaaniye nitamlaani; na katika wewe jamaa zote za dunia watabarikiwa.
Mungu akasema, Sivyo, lakini Sara mkeo atakuzalia mwana wa kiume, nawe utamwita jina lake Isaka. Nami nitafanya agano langu imara kwake kuwa agano la milele kwa ajili ya uzao wake baada yake.
Agano langu nitalifanya imara kati yangu na wewe, na uzao wako baada yako, na vizazi vyao, kuwa agano la milele, kwamba nitakuwa Mungu kwako na kwa uzao wako baada yako.
Nitazidisha uzao wako kama nyota za mbinguni, nami nitawapa uzao wako nchi hizi zote, na katika uzao wako mataifa yote ya dunia watajibarikia.
Na uzao wako utakuwa kama mavumbi ya nchi, nawe utaenea upande wa magharibi, na mashariki, na kaskazini, na kusini; na katika wewe, na katika uzao wako, jamaa zote za dunia watabarikiwa.