Neno la BWANA kwa Bwana wangu, Uketi upande wangu wa kulia, Hadi niwafanyapo adui zako Kuwa chini ya miguu yako.
Luka 1:43 - Swahili Revised Union Version Limenitokeaje neno hili, hata mama wa Bwana wangu anijie mimi? Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mimi ni nani hata mama wa Bwana wangu afike kwangu? Biblia Habari Njema - BHND Mimi ni nani hata mama wa Bwana wangu afike kwangu? Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mimi ni nani hata mama wa Bwana wangu afike kwangu? Neno: Bibilia Takatifu Lakini ni kwa nini mimi nimepata kibali kiasi hiki, hata mama wa Bwana wangu afike kwangu? Neno: Maandiko Matakatifu Lakini ni kwa nini mimi nimepata upendeleo kiasi hiki, hata mama wa Bwana wangu afike kwangu? BIBLIA KISWAHILI Limenitokeaje neno hili, hata mama wa Bwana wangu anijie mimi? |
Neno la BWANA kwa Bwana wangu, Uketi upande wangu wa kulia, Hadi niwafanyapo adui zako Kuwa chini ya miguu yako.
Alipokuwa katika kusema na makutano, tazama, mama yake na ndugu zake walikuwa wakisimama nje, wataka kusema naye.
Lakini Yohana alitaka kumzuia, akisema, Mimi nahitaji kubatizwa na wewe, nawe waja kwangu?
akapaza sauti kwa nguvu akasema, Umebarikiwa wewe katika wanawake, naye mzao wa tumbo lako amebarikiwa.
Maana sauti ya kuamkia kwako ilipoingia masikioni mwangu, kitoto kichanga kikaruka kwa shangwe ndani ya tumbo langu.
kwa hiyo nilijiona sistahili mwenyewe kuja kwako; lakini, sema neno tu, na mtumwa wangu atapona.
Msitende neno lolote kwa kushindana wala kwa majivuno; bali kwa unyenyekevu, kila mtu na amhesabu mwenziwe kuwa bora kuliko nafsi yake.
Naam, zaidi ya hayo, nayahesabu mambo yote kuwa hasara kwa ajili ya uzuri usio na kiasi wa kumjua Kristo Yesu, Bwana wangu; ambaye kwa ajili yake nimepata hasara ya mambo yote nikiyahesabu kuwa kama mavi ili nipate Kristo;
Ndipo aliposujudia, akainama mpaka nchi, akamwambia, Jinsi gani nimepata kibali machoni pako, hata ukanifahamu, mimi niliye mgeni?
Naye akainuka na kujiinamisha kifudifudi mpaka chini, akasema, Tazama, mjakazi wako ni mtumishi wa kuwaosha miguu watumishi wa bwana wangu.