Kutoka 1:8 - Swahili Revised Union Version Basi akatokea mfalme mpya kutawala Misri, asiyemjua Yusufu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Basi, akatokea mfalme mwingine huko Misri ambaye hakumjua Yosefu. Biblia Habari Njema - BHND Basi, akatokea mfalme mwingine huko Misri ambaye hakumjua Yosefu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Basi, akatokea mfalme mwingine huko Misri ambaye hakumjua Yosefu. Neno: Bibilia Takatifu Kisha mfalme mwingine ambaye hakufahamu habari za Yusufu akatawala Misri. Neno: Maandiko Matakatifu Kisha mfalme mpya ambaye hakufahamu habari za Yusufu akatawala Misri. BIBLIA KISWAHILI Basi akatokea mfalme mpya kutawala Misri, asiyemjua Yusufu. |
Nenda, ukawakusanye wazee wa Israeli pamoja, ukawaambie, BWANA, Mungu wa baba zenu, Mungu wa Abrahamu, Mungu wa Isaka, Mungu wa Yakobo, amenitokea, akaniambia, Hakika nimewajilieni, tena nimeyaona mnayotendewa huko Misri;
BWANA akasema, Hakika nimeyaona mateso ya watu wangu walioko Misri, nami nimekisikia kilio chao kwa sababu ya wasimamizi wao; maana nayajua maumivu yao;
Basi, tazama, kilio cha wana wa Israeli kimenifikia; tena nimeyaona hayo mateso ambayo Wamisri wanawatesa.
Basi, kulikuwemo na mtu maskini mwenye hekima, naye kwa hekima yake akauokoa mji ule lakini hata hivyo hapakuwa na mtu yeyote aliyemkumbuka yule mtu maskini.
Huyo akawafanyia hila kabila yetu, na kuwatenda mabaya baba zetu, akiwaamuru wawatupe watoto wao wachanga, ili wasiishi.
Tena watu wote wa kizazi hicho nao walikusanywa waende kwa baba zao; kikainuka kizazi kingine nyuma yao, ambacho hakikumjua BWANA, wala hawakuijua hiyo kazi ambayo alikuwa ameitenda kwa ajili ya Israeli.