Mbona mnataka kupigwa, hata sasa, hata mkazidi kuasi? Kichwa chote ni kigonjwa, moyo wote umezimia.
Isaya 7:20 - Swahili Revised Union Version Katika siku hiyo Bwana atanyoa kichwa na malaika ya miguuni, kwa wembe ulioajiriwa pande za ng'ambo ya Mto, yaani, kwa mfalme wa Ashuru, nao utaziondoa ndevu pia. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wakati huo, Bwana atakopa wembe kutoka ngambo ya mto Eufrate, yaani mfalme wa Ashuru. Atawanyoa vichwa vyenu, miili yenu na kukatilia mbali pia ndevu zenu. Biblia Habari Njema - BHND Wakati huo, Bwana atakopa wembe kutoka ngambo ya mto Eufrate, yaani mfalme wa Ashuru. Atawanyoa vichwa vyenu, miili yenu na kukatilia mbali pia ndevu zenu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wakati huo, Bwana atakopa wembe kutoka ng'ambo ya mto Eufrate, yaani mfalme wa Ashuru. Atawanyoa vichwa vyenu, miili yenu na kukatilia mbali pia ndevu zenu. Neno: Bibilia Takatifu Katika siku ile Bwana atatumia wembe ulioajiriwa kutoka ng’ambo ya Mto, yaani mfalme wa Ashuru, kunyoa nywele za kichwa chako na malaika ya miguu yako, na kuziondoa ndevu zako pia. Neno: Maandiko Matakatifu Katika siku ile Bwana atatumia wembe ulioajiriwa kutoka ng’ambo ya Mto, yaani mfalme wa Ashuru, kunyoa nywele za kichwa chako na malaika ya miguu yako, na kuziondoa ndevu zako pia. BIBLIA KISWAHILI Katika siku hiyo Bwana atanyoa kichwa na malaika ya miguuni, kwa wembe ulioajiriwa pande za ng'ambo ya Mto, yaani, kwa mfalme wa Ashuru, nao utaziondoa ndevu pia. |
Mbona mnataka kupigwa, hata sasa, hata mkazidi kuasi? Kichwa chote ni kigonjwa, moyo wote umezimia.
Je! Shoka lijisifu juu yake alitumiaye? Je! Msumeno ujitukuze juu yake auvutaye? Ingekuwa kana kwamba bakora ingewatikisa waiinuao, au fimbo ingemwinua yeye ambaye si mti.
Na BWANA atauangamiza kabisa ulimi wa bahari ya Misri; na kwa upepo wake uteketezao atatikisa mkono wake juu ya Mto, naye ataupiga, uwe vijito saba, na kuwavusha watu waliovaa viatu bila kulowa.
Ikawa, katika mwaka wa kumi na nne wa kutawala kwake mfalme Hezekia, Senakeribu, mfalme wa Ashuru, akapanda ili kupigana na miji yote ya Yuda yenye boma, akaitwaa.
basi sasa angalia; Bwana aleta juu yao maji ya huo Mto, yenye nguvu, mengi sana, nayo ni mfalme wa Ashuru na utukufu wake wote; naye atakuja, na kupita juu ya mifereji yake yote, atafurika juu ya kingo zake zote;
Na sasa una nini utakayofaidi katika njia iendayo Misri, kunywa maji ya Shihori? Au una nini utakayofaidi katika njia iendayo Ashuru, kunywa maji ya ule Mto?
Mwanadamu, Nebukadneza, mfalme wa Babeli, alilifanyisha jeshi lake kazi ngumu juu ya Tiro; kila kichwa kilitiwa upara, na kila bega liliambuliwa ngozi, lakini hakuna mshahara uliotoka Tiro, sio wake wala wa jeshi lake, kwa kazi ile aliyofanya juu yake.
Nimempa nchi ya Misri kuwa malipo ya kazi aliyofanya, kwa sababu walifanya kazi kwa ajili yangu; asema Bwana MUNGU.