Isaya 64:12 - Swahili Revised Union Version Utajizuia usiyaangalie mambo haya, Ee BWANA? Utanyamaza, na kutuadhibu vikali? Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Je, kwa hayo yote utajizuia usifanye kitu? Je, utaendelea kunyamaza tu, ee Mwenyezi-Mungu, na kututesa kupita kiasi? Biblia Habari Njema - BHND Je, kwa hayo yote utajizuia usifanye kitu? Je, utaendelea kunyamaza tu, ee Mwenyezi-Mungu, na kututesa kupita kiasi? Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Je, kwa hayo yote utajizuia usifanye kitu? Je, utaendelea kunyamaza tu, ee Mwenyezi-Mungu, na kututesa kupita kiasi? Neno: Bibilia Takatifu Ee Mwenyezi Mungu, baada ya haya yote, utajizuia? Je, utanyamaza, na kutuadhibu kupita kiasi? Neno: Maandiko Matakatifu Ee bwana, baada ya haya yote, utajizuia? Je, utanyamaza kimya na kutuadhibu kupita kiasi? BIBLIA KISWAHILI Utajizuia usiyaangalie mambo haya, Ee BWANA? Utanyamaza, na kutuadhibu vikali? |
Siku nyingi nimenyamaza kimya; nimenyamaza, nikajizuia; sasa nitapiga kelele kama mwanamke aliye katika kuzaa; nitaugua na kutweta pamoja.
Tazama toka mbinguni, ukaone toka makao ya utukufu wako na fahari yako; uko wapi wivu wako, na uweza wako? Shauku ya moyo wako, na huruma zako zimezuiliwa kwangu.
Tazama, neno hili limeandikwa mbele zangu. Sitanyamaza, lakini nitalipa, naam, mimi nitawalipa ujira wao vifuani mwao;
Ndipo yule malaika wa BWANA akajibu, akasema, Ee BWANA wa majeshi, hadi lini utakataa kuurehemu Yerusalemu, na miji ya Yuda uliyoikasirikia miaka hii sabini?
Wakalia kwa sauti kuu, wakisema, Ee Mola, Mtakatifu, na Mkweli, utakawia hadi lini kuhukumu na kuilipa damu yetu kwa hao wakaao juu ya nchi?