Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Isaya 42:14 - Swahili Revised Union Version

14 Siku nyingi nimenyamaza kimya; nimenyamaza, nikajizuia; sasa nitapiga kelele kama mwanamke aliye katika kuzaa; nitaugua na kutweta pamoja.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

14 Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Kwa muda mrefu sasa nimenyamaza, nimekaa kimya na kujizuia; lakini sasa nitalia kama mama anayejifungua, anayetweta pamoja na kuhema.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

14 Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Kwa muda mrefu sasa nimenyamaza, nimekaa kimya na kujizuia; lakini sasa nitalia kama mama anayejifungua, anayetweta pamoja na kuhema.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

14 Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Kwa muda mrefu sasa nimenyamaza, nimekaa kimya na kujizuia; lakini sasa nitalia kama mama anayejifungua, anayetweta pamoja na kuhema.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

14 “Kwa muda mrefu nimenyamaza; nimekaa kimya na kujizuia. Lakini sasa, kama mwanamke wakati wa kujifungua, ninapiga kelele, ninatweta na kushusha pumzi.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

14 “Kwa muda mrefu nimenyamaza kimya, nimekaa kimya na kujizuia. Lakini sasa, kama mwanamke wakati wa kujifungua, ninapiga kelele, ninatweta na kushusha pumzi.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

14 Siku nyingi nimenyamaza kimya; nimenyamaza, nikajizuia; sasa nitapiga kelele kama mwanamke aliye katika kuzaa; nitaugua na kutweta pamoja.

Tazama sura Nakili




Isaya 42:14
16 Marejeleo ya Msalaba  

Kwa kuwa nimejaa maneno; Roho iliyo ndani yangu hunihimiza.


Nitanena, ili nipate kutulia; Nitafunua midomo yangu na kujibu.


Tokea Sayuni, ukamilifu wa uzuri, Mungu ameangaza kote.


Ndivyo ulivyofanya, nami nikanyamaza; Ukadhani ya kuwa Mimi ni kama wewe. Lakini nitakukemea; Nitakuhukumu kwa hayo yote.


Kwa ajili ya hayo BWANA atangoja, ili awaonee huruma, na kwa ajili ya hayo atatukuzwa, ili awarehemu; kwa maana BWANA ni Mungu wa hukumu; heri wote wamngojao.


Tena ni nani uliyemwogopa na kumhofu, hata ukasema uongo, wala hukunikumbuka mimi, wala kuweka hayo moyoni? Je! Mimi sikunyamaza tangu zamani, hata huniogopi?


Utajizuia usiyaangalie mambo haya, Ee BWANA? Utanyamaza, na kutuadhibu vikali?


Tazama, neno hili limeandikwa mbele zangu. Sitanyamaza, lakini nitalipa, naam, mimi nitawalipa ujira wao vifuani mwao;


Umenikataa mimi, asema BWANA, umerudi nyuma; ndiyo maana nimenyosha mkono wangu juu yako, na kukuangamiza; nimechoka kwa kughairi.


Kwa maana nimesikia sauti, kama sauti ya mwanamke wakati wa uchungu wake, na sauti yake aumwaye, kama mwanamke azaaye mtoto wake wa kwanza, sauti ya binti Sayuni, atwetaye kupata pumzi, na kunyosha mikono yake, akisema, Ole wangu, sasa! Kwa maana roho yangu inazimia mbele ya wauaji.


Hata BWANA asiweze kuvumilia tena, kwa sababu ya uovu wa matendo yenu, na kwa sababu ya machukizo mliyoyafanya; kwa sababu hiyo nchi yenu imekuwa ukiwa, na ajabu, na laana, isikaliwe na mtu kama ilivyo leo.


Na Mungu, je! Hatawapatia haki wateule wake wanaomlilia mchana na usiku, naye ni mvumilivu kwao?


Nanyi uhesabuni uvumilivu wa Bwana wetu kuwa ni wokovu, kama vile na ndugu yetu mpenzi Paulo alivyowaandikia kwa hekima aliyopewa;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo