Biblia ya mtandaoni

Matangazo

Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya

Isaya 59:5 - Swahili Revised Union Version

Huangua mayai ya fira, na kusuka wavu wa buibui; yeye alaye mayai yao hufa, na hilo livunjwalo hutoka nyoka.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Mnaangua mayai ya joka lenye sumu, mnafuma utando wa buibui. Anayekula mayai yenu hufa, na yakipasuliwa nyoka hutokea.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Mnaangua mayai ya joka lenye sumu, mnafuma utando wa buibui. Anayekula mayai yenu hufa, na yakipasuliwa nyoka hutokea.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Mnaangua mayai ya joka lenye sumu, mnafuma utando wa buibui. Anayekula mayai yenu hufa, na yakipasuliwa nyoka hutokea.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Huangua mayai ya nyoka wenye sumu kali na kutanda wavu wa buibui. Yeyote alaye mayai yao atakufa, nalo moja likianguliwa, nyoka hutoka humo.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Huangua mayai ya nyoka wenye sumu kali na kutanda wavu wa buibui. Yeyote alaye mayai yao atakufa, na wakati moja lianguliwapo, nyoka hutoka humo.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Huangua mayai ya fira, na kusuka wavu wa buibui; yeye alaye mayai yao hufa, na hilo livunjwalo hutoka nyoka.

Tazama sura
Tafsiri zingine

Isaya 59:5
6 Marejeleo ya Msalaba  

Uthabiti wake utavunjika, Na matumaini yake huwa ni utando wa buibui.

Mwisho wake huuma kama nyoka; Huchoma kama fira.

Msifurahi, Enyi Wafilisti wote, Kwa sababu fimbo ile iliyokupiga imevunjika; Maana katika shina la nyoka atatoka fira, Na uzao wake ni joka la moto arukaye Sef 2:4-7; Zek 9:5-7

Huko bundi atajenga kiota chake na kutaga mayai na kuyaatamia, na kuangua, na kukusanya vifaranga wake katika kivuli chake; naam, huko watakusanyika tai, kila mmoja na mwenzake.

Enyi wazawa wa nyoka, mwawezaje kunena mema, mkiwa wabaya? Maana, kinywa cha mtu huyanena yaujazayo moyo wake.

Na alipoona wengi miongoni mwa Mafarisayo na Masadukayo wakiujia ubatizo wake, aliwaambia, Enyi wazawa wa nyoka, ni nani aliyewaonya ninyi kuikimbia hasira itakayokuja?