Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Isaya 59:6 - Swahili Revised Union Version

6 Nyavu zao hazitakuwa mavazi, wala hawatajifunika kwa kazi zao; kazi zao ni kazi za uovu, na vitendo vya udhalimu vimo mikononi mwao.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

6 Utando wenu haufai kwa mavazi, watu hawawezi kujifunikia mnachofuma. Kazi zenu ni kazi za uovu, matendo yenu yote ni ukatili mtupu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

6 Utando wenu haufai kwa mavazi, watu hawawezi kujifunikia mnachofuma. Kazi zenu ni kazi za uovu, matendo yenu yote ni ukatili mtupu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

6 Utando wenu haufai kwa mavazi, watu hawawezi kujifunikia mnachofuma. Kazi zenu ni kazi za uovu, matendo yenu yote ni ukatili mtupu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

6 Utando wao wa buibui haufai kwa mavazi; hawawezi kujifunika kwa kile walichokitengeneza. Matendo yao ni matendo maovu, vitendo vya jeuri vipo mikononi mwao.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

6 Utando wao wa buibui haufai kwa nguo; hawawezi kujifunika kwa kile walichokitengeneza. Matendo yao ni matendo maovu, vitendo vya jeuri vipo mikononi mwao.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

6 Nyavu zao hazitakuwa mavazi, wala hawatajifunika kwa kazi zao; kazi zao ni kazi za uovu, na vitendo vya udhalimu vimo mikononi mwao.

Tazama sura Nakili




Isaya 59:6
31 Marejeleo ya Msalaba  

Dunia ikaharibika mbele za Mungu, dunia ikajaa dhuluma.


Ijapokuwa hakuna udhalimu mikononi mwangu, Na kuomba kwangu ni safi.


Tamaa mbaya zimo ndani yake; Dhuluma na hila haziondoki mitaani mwake.


Sivyo! Mioyoni mwenu mnatenda maovu; Mikono yenu wenyewe inaeneza udhalimu katika nchi.


Ole wa watoto waasi; asema BWANA; watakao mashauri lakini hawayataki kwangu mimi; wajifunikao kifuniko lakini si cha roho yangu; wapate kuongeza dhambi juu ya dhambi;


Kwa maana shamba la mizabibu la BWANA wa majeshi ndilo nyumba ya Israeli, na watu wa Yuda ni mche wake wa kupendeza; akatumaini kuona hukumu ya haki, na kumbe! Aliona dhuluma; alitumaini kuona haki, na kumbe! Alisikia kilio.


Mimi nitatangaza haki yako, na matendo yako hayatakufaa.


Tazama, ninyi mnafunga ili mpate kushindana na kugombana, na kupiga kwa ngumi ya uovu. Kufunga kama huku kwa siku ya leo hakutafanya sauti zenu zisikike juu.


Kwa maana sisi sote tumekuwa kama mtu aliye mchafu, na matendo yetu yote ya haki yamekuwa kama nguo iliyotiwa unajisi; sisi sote twanyauka kama jani, na maovu yetu yatuondoa, kama upepo uondoavyo.


Kama vile kisima kitoavyo maji yake, ndivyo utoavyo uovu wake; jeuri na kuharibu kwasikiwa ndani yake; ugonjwa na jeraha zi mbele zangu daima.


na kuwadhulumu maskini na wahitaji, na kuwanyang'anya watu mali yao kwa nguvu, wala hakurudisha rehani, naye ameviinulia macho vinyago, na kufanya machukizo,


Udhalimu umeinuka, ukawa fimbo ya uovu; hapana mtu atakayesalia miongoni mwao, wala katika jamii yao, wala kitu katika utajiri wao; wala hakutakuwa kutukuka kati yao.


Ufue mnyororo; kwa maana nchi hii imejaa hukumu za damu, nao mji umejaa udhalimu.


Ndipo akaniambia, Uovu wa nyumba ya Israeli na Yuda ni mwingi sana, nayo nchi imejaa damu, nao mji umejaa kupotosha hukumu; maana husema, BWANA ameiacha nchi hii, naye BWANA haoni.


Kwa maana hawajui kutenda haki, asema BWANA, hao wawekao akiba ya jeuri na unyang'anyi katika majumba yao.


Ninyi mnaoiweka mbali siku hiyo mbaya, na kulileta karibu kao la udhalimu;


Lakini siku hizi mmeinuka kama adui za watu wangu; mnawapokonya joho lililo juu ya nguo za hao wapitao salama bila kutarajia vita.


Kwa maana matajiri wake wamejaa jeuri, na wenyeji wake wamesema uongo, na ulimi wao una udanganyifu kichwani mwao.


Na katika siku ile nitawaadhibu hao wote warukao juu ya kizingiti, waijazao nyumba ya bwana wao udhalimu na udanganyifu.


Ole wake yeye aliyeasi na kutiwa unajisi, mji wa udhalimu!


Maana mimi nakuchukia kuachana, asema BWANA, Mungu wa Israeli; naye aifunikizaye nguo yake kwa udhalimu namchukia, asema BWANA wa majeshi; basi jihadharini roho zenu, msije mkatenda kwa hiana.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo