Nayo nchi ilikuwa tupu, tena bila umbo, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji.
Isaya 40:13 - Swahili Revised Union Version Ni nani aliyemwongoza Roho ya BWANA, na kumfundisha kwa kuwa mshauri wake? Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Nani awezaye kuiongoza akili ya Mwenyezi-Mungu, au kuwa mshauri wake na kumfunza? Biblia Habari Njema - BHND Nani awezaye kuiongoza akili ya Mwenyezi-Mungu, au kuwa mshauri wake na kumfunza? Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Nani awezaye kuiongoza akili ya Mwenyezi-Mungu, au kuwa mshauri wake na kumfunza? Neno: Bibilia Takatifu Ni nani aliyeyafahamu mawazo ya Mwenyezi Mungu, au kumfundisha akiwa kama mshauri wake? Neno: Maandiko Matakatifu Ni nani aliyeyafahamu mawazo ya bwana, au kumfundisha akiwa kama mshauri wake? BIBLIA KISWAHILI Ni nani aliyemwongoza Roho ya BWANA, na kumfundisha kwa kuwa mshauri wake? |
Nayo nchi ilikuwa tupu, tena bila umbo, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji.
Na nitazamapo, hapana mtu, hata katika watu hao hapana mshauri mmoja, ambaye, nikimwuliza, aweza kunijibu neno.
Maana, ni nani aliyesimama katika baraza la BWANA, hata akalifahamu neno lake na kulisikia? Ni nani aliyelitia moyoni neno langu, na kulisikia?
Akasema, Nimekabidhiwa vyote na Baba yangu, wala hakuna amjuaye Mwana ila Baba; wala hakuna amjuaye Baba ila Mwana, na yeyote ambaye Mwana apenda kumfunulia.
waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu.
Maana, Ni nani aliyeifahamu nia ya Bwana, amwelimishe? Lakini sisi tunayo nia ya Kristo.
na ndani yake sisi nasi tulifanywa urithi, huku tukichaguliwa tangu awali sawasawa na kusudi lake yeye, ambaye hufanya mambo yote kwa shauri la mapenzi yake.