Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Mwanzo 1:2 - Swahili Revised Union Version

2 Nayo nchi ilikuwa tupu, tena bila umbo, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

2 Dunia ilikuwa bila umbo na tupu. Giza lilikuwa limefunika vilindi vya maji na roho ya Mungu ilikuwa ikitanda juu ya maji.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

2 Dunia ilikuwa bila umbo na tupu. Giza lilikuwa limefunika vilindi vya maji na roho ya Mungu ilikuwa ikitanda juu ya maji.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

2 Dunia ilikuwa bila umbo na tupu. Giza lilikuwa limefunika vilindi vya maji na roho ya Mungu ilikuwa ikitanda juu ya maji.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

2 Wakati huu dunia ilikuwa haina umbo, tena ilikuwa tupu. Giza lilikuwa juu ya vilindi vya maji, naye Roho wa Mungu alikuwa ametulia juu ya maji.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

2 Wakati huu dunia ilikuwa haina umbo, tena ilikuwa tupu. Giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji, naye Roho wa Mwenyezi Mungu alikuwa ametulia juu ya maji.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

2 Nayo nchi ilikuwa tupu, tena bila umbo, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji.

Tazama sura Nakili




Mwanzo 1:2
17 Marejeleo ya Msalaba  

Tazama, hivi ni viunga tu vya njia zake; Na jinsi yalivyo madogo manong'ono tusikiayo katika habari zake! Lakini ngurumo za uweza wake ni nani awezaye kuzielewa?


Yeye hutandaza kaskazi juu ya nafasi isiyo na kitu, Na kuutundika ulimwengu pasipo kitu.


Nilipolifanya wingu kuwa vazi lake, Na giza zito kuwa nguo ya kuifungia,


Hufanya mapito yake kung'aa nyuma yake Hata mtu angedhani kilindi kina mvi.


Waituma roho yako, wanaumbwa, Nawe waufanya upya uso wa nchi.


Uliifunika kwa vilindi kama kwa vazi, Maji yalikuwa yakisimama juu ya milima.


Yeye aliyeitandaza nchi juu ya maji; Kwa maana fadhili zake ni za milele.


Msifuni BWANA kutoka nchi, Enyi nyangumi na vilindi vyote.


Kwa neno la BWANA mbingu ziliumbwa, Na jeshi lake lote kwa pumzi ya kinywa chake.


Wakati havijakuwapo vilindi nilizaliwa, Wakati hazijakuwapo chemchemi zilizojaa maji.


Kama ndege warukao, BWANA wa majeshi ataulinda Yerusalemu; ataulinda na kuuokoa, atapita juu yake na kuuhifadhi.


Maana BWANA, aliyeziumba mbingu, asema hivi; Yeye ni Mungu; ndiye aliyeiumba dunia na kuifanya; ndiye aliyeifanya imara; hakuiumba iwe ukiwa, aliiumba ili ikaliwe na watu; Mimi ni BWANA, wala hapana mwingine.


Niliiangalia nchi, na tazama, ilikuwa ukiwa, haina watu; niliziangalia mbingu, nazo zilikuwa hazina nuru.


Amekuwa utupu, na ukiwa, na uharibifu; hata moyo unayeyuka, na magoti yanagonganagongana; moyoni kote mna uchungu, na nyuso za wote zimekuwa nyeupe kwa hofu.


Kwa kuwa Mungu, aliyesema, Nuru itang'aa toka gizani, ndiye aliyeng'aa mioyoni mwetu, atupe nuru ya elimu ya utukufu wa Mungu katika uso wa Yesu Kristo.


Mfano wa tai ataharikishaye kioto chake; Na kupapatika juu ya makinda yake, Alikunjua mbawa zake, akawatwaa, Akawachukua juu ya mbawa zake;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo