Isaya 38:11 - Swahili Revised Union Version Nilisema, Sitamwona BWANA, yeye BWANA, katika nchi ya walio hai; Sitamwona mwanadamu tena pamoja na hao wakaao duniani. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Nilisema sitamwona tena Mwenyezi-Mungu, katika nchi ya walio hai; wala sitamwona mtu yeyote tena, miongoni mwa wakazi wa ulimwengu. Biblia Habari Njema - BHND Nilisema sitamwona tena Mwenyezi-Mungu, katika nchi ya walio hai; wala sitamwona mtu yeyote tena, miongoni mwa wakazi wa ulimwengu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Nilisema sitamwona tena Mwenyezi-Mungu, katika nchi ya walio hai; wala sitamwona mtu yeyote tena, miongoni mwa wakazi wa ulimwengu. Neno: Bibilia Takatifu Nilisema, “Sitamwona tena Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu katika nchi ya walio hai, wala sitamtazama tena mwanadamu, wala kuwa na wale ambao sasa wanakaa katika ulimwengu huu. Neno: Maandiko Matakatifu Nilisema, “Sitamwona tena bwana, bwana katika nchi ya walio hai, wala sitamtazama tena mwanadamu, wala kuwa na wale ambao sasa wanakaa katika ulimwengu huu. BIBLIA KISWAHILI Nilisema, Sitamwona BWANA, yeye BWANA, katika nchi ya walio hai; Sitamwona mwanadamu tena pamoja na hao wakaao duniani. |
Nami nilisema kwa pupa yangu, Nimekatiliwa mbali na macho yako; Lakini ulisikia sauti ya kilio changu Wakati nilipokulilia.
Elamu yuko huko, na watu wake umati wote, pande zote za kaburi lake; wote pia wameuawa, wameanguka kwa upanga, walioshuka wakiwa hawajatahiriwa hadi pande za chini ya nchi; ambao waliwatia watu hofu katika nchi ya walio hai, nao wamechukua aibu yao, pamoja nao washukao shimoni.