Biblia ya mtandaoni

Matangazo


Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya




Isaya 37:1 - Swahili Revised Union Version

Ikawa mfalme Hezekia aliposikia hayo, alizirarua nguo zake, akajivika nguo za magunia, akaingia katika nyumba ya BWANA.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Basi, mfalme Hezekia aliposikia habari hiyo alirarua mavazi yake, akavaa vazi la gunia, akaingia katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Basi, mfalme Hezekia aliposikia habari hiyo alirarua mavazi yake, akavaa vazi la gunia, akaingia katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Basi, mfalme Hezekia aliposikia habari hiyo alirarua mavazi yake, akavaa vazi la gunia, akaingia katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Mfalme Hezekia aliposikia haya, akararua nguo zake na kuvaa gunia, na akaenda katika Hekalu la Mwenyezi Mungu.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Mfalme Hezekia aliposikia haya, akararua nguo zake na kuvaa nguo ya gunia, naye akaenda katika Hekalu la bwana.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Ikawa mfalme Hezekia aliposikia hayo, alizirarua nguo zake, akajivika nguo za magunia, akaingia katika nyumba ya BWANA.

Tazama sura
Tafsiri zingine



Isaya 37:1
13 Marejeleo ya Msalaba  

Ikawa, mfalme alipokwisha kuyasikia maneno ya kitabu hicho cha torati, alirarua nguo zake.


Na kwa ajili ya hayo Hezekia mfalme, na Isaya nabii, mwana wa Amozi, wakaomba, wakalia hata mbinguni.


Na wakati wa sadaka ya jioni nikainuka baada ya kunyenyekea kwangu, nguo yangu na joho langu zimeraruliwa, nikaanguka magotini nikakunjua mikono yangu mbele za BWANA, Mungu wangu;


Basi Mordekai alipojua mambo yote yaliyofanyika, alizirarua nguo zake, akajivika gunia na kujipaka majivu, akatoka hadi katikati ya mji, akalia kwa sauti kuu ya uchungu.


Siku hiyo Bwana, BWANA wa majeshi, akawaita watu walie na kuomboleza, na kung'oa nywele zao, na kuvaa nguo za magunia;


Ndipo Eliakimu, mwana wa Hilkia, aliyekuwa msimamizi wa nyumba ya mfalme, na Shebna, mwandishi, na Yoa, mwana wa Asafu mwenye kuandika kumbukumbu, wakaenda kwa Hezekia, na nguo zao zikiwa zimeraruliwa, wakamwambia Hezekia maneno ya yule kamanda.


Basi Hezekia akaupokea waraka katika mikono ya wale wajumbe, akausoma; kisha Hezekia akapanda, akaingia katika nyumba ya BWANA, akaukunjua mbele za BWANA.


Je! Hezekia, mfalme wa Yuda, na watu wote wa Yuda, walimwua Mikaya? Je! Hakumcha BWANA, na kumwomba BWANA awafadhili; naye BWANA akaghairi, asiyatende mabaya yale aliyoyatamka juu yao? Lakini sisi tuko karibu kujiletea maafa makuu wenyewe.


Lakini hawakuogopa, wala hawakurarua mavazi yao, wala mfalme, wala watumishi wake hata mmoja waliosikia maneno hayo yote.


Ole wako, Korazini! Ole wako, Bethsaida! Kwa kuwa kama miujiza iliyofanyika kwenu ingalifanyika katika Tiro na Sidoni, wangalitubu zamani kwa kuvaa magunia na majivu.