Asa na watu waliokuwa pamoja naye wakawafuata mpaka Gerari; wakawaua Wakushi wengi sana asipone hata mmoja; kwa sababu waliangamizwa mbele za BWANA, na mbele ya jeshi lake; na hao wakachukua mateka wengi sana.
Isaya 33:4 - Swahili Revised Union Version Na mateka yako yatakukusanywa kama wadudu wakumbavyo, wataruka juu yake kama arukavyo nzige. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Maadui zao wanakusanya mateka, wanayarukia kama panzi. Biblia Habari Njema - BHND Maadui zao wanakusanya mateka, wanayarukia kama panzi. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Maadui zao wanakusanya mateka, wanayarukia kama panzi. Neno: Bibilia Takatifu Mateka yenu, enyi mataifa, yamevunwa kama wafanyavyo madumadu, watu huvamia juu yake kama kundi la nzige. Neno: Maandiko Matakatifu Mateka yenu, enyi mataifa, yamevunwa kama vile wafanyavyo madumadu, kama kundi la nzige watu huvamia juu yake. BIBLIA KISWAHILI Na mateka yako yatakusanywa kama wadudu wakumbavyo, wataruka juu yake kama arukavyo nzige. |
Asa na watu waliokuwa pamoja naye wakawafuata mpaka Gerari; wakawaua Wakushi wengi sana asipone hata mmoja; kwa sababu waliangamizwa mbele za BWANA, na mbele ya jeshi lake; na hao wakachukua mateka wengi sana.
Nao Yehoshafati na watu wake walipokuja kuchukua nyara zao, wakakuta miongoni mwao mifugo wengi sana, mali, mavazi na vitu vya thamani, walivyojinyakulia, zaidi kuliko wawezavyo kuchukua; wakawa siku tatu katika kuteka nyara, maana zilikuwa nyingi sana.
Kamba zako zimelegea; hawakuweza kukaza sana shina la mlingoti wao; hawakuweza kulikunjua tanga; ndipo mapato ya mateka yaligawanywa, hata wachechemeao walipata mateka.
Makabila ya watu wamekimbia wakisikia kelele za fujo; mataifa wametawanyika ulipojiinua nafsi yako.
basi, tazama, nimenyosha mkono wangu juu yako, nami nitakutoa uwe mateka ya mataifa; nami nitakukatilia mbali na makabila ya watu, nami nitakuangamiza, usiwe katika nchi hizo; nitakukomesha; nawe utajua ya kuwa mimi ndimi BWANA.
Yaliyosazwa na tunutu yameliwa na nzige; na yaliyosazwa na nzige yameliwa na parare; na yaliyosazwa na parare yameliwa na madumadu.
Nami nitawarudishia hiyo miaka iliyoliwa na nzige, na parare, na madumadu, na tunutu, jeshi langu kubwa nililotuma kati yenu.
Moto unaunguza vikali mbele yao; na nyuma yao miali ya moto inateketeza; hiyo nchi inafanana na bustani ya Edeni mbele yao, na nyuma yao imekuwa jangwa tupu; naam, hakuna aliyeokoka asipatikane nao.
Huurukia mji; hupiga mbio juu ya ukuta; hupanda na kuingia ndani ya nyumba; huingia madirishani kama aingiavyo mwizi.