Kwa ajili ya kuonewa kwao wanyonge, Kwa ajili ya kuugua kwao wahitaji, Sasa nitasimama, asema BWANA, Nitamweka salama yeye wanayemfyonya.
Isaya 33:10 - Swahili Revised Union Version Basi, sasa nitasimama; asema BWANA; sasa nitajiinua, sasa nitajitukuza. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Sasa mimi nitainuka; sasa nitajiweka tayari; sasa mimi nitatukuzwa. Biblia Habari Njema - BHND Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Sasa mimi nitainuka; sasa nitajiweka tayari; sasa mimi nitatukuzwa. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Sasa mimi nitainuka; sasa nitajiweka tayari; sasa mimi nitatukuzwa. Neno: Bibilia Takatifu “Sasa nitainuka,” asema Mwenyezi Mungu. “Sasa nitatukuzwa; sasa nitainuliwa juu. Neno: Maandiko Matakatifu “Sasa nitainuka,” asema bwana. “Sasa nitatukuzwa; sasa nitainuliwa juu. BIBLIA KISWAHILI Basi, sasa nitasimama; asema BWANA; sasa nitajiinua, sasa nitajitukuza. |
Kwa ajili ya kuonewa kwao wanyonge, Kwa ajili ya kuugua kwao wahitaji, Sasa nitasimama, asema BWANA, Nitamweka salama yeye wanayemfyonya.
Maneno ya BWANA ni maneno safi, Ni fedha iliyojaribiwa kalibuni juu ya nchi; Iliyosafishwa mara saba.
BWANA uondoke kwa hasira yako; Ujiinue Juu ya ujeuri wa watesi wangu; Uamke kwa ajili yangu; Umeamuru hukumu.
Ndipo Bwana alipoamka kama aliyelala usingizi, Kama shujaa apigaye kelele kwa sababu ya mvinyo;
Ni nani atakayesimama Kwa ajili yangu juu ya wabaya? Ni nani atakayenisaidia Juu yao wafanyao maovu?
Na Wamisri watajua ya kuwa mimi ndimi BWANA, nitakapokwisha kujipatia utukufu kwa Farao, na magari yake, na farasi wake.
Kwa hiyo Bwana, BWANA wa majeshi, atatuma maradhi ya kukondesha kwa wapiganaji walionenepa; na badala ya utukufu wake kutawashwa kuteketea kama kuteketea kwa moto.
Angalia, Bwana, BWANA wa majeshi, atayakata matawi kwa nguvu za kutisha; nao walio warefu wa kimo watakatwa; na hao walioinuka wataangushwa chini;
Na watu wataingia ndani ya pango za majabali, na ndani ya mashimo ya nchi, mbele za utisho wa BWANA na utukufu wa enzi yake, atakapoondoka ili aitetemeshe mno dunia.
ili aingie ndani ya pango za majabali, na ndani ya tundu za miamba iliyopasuka, mbele za utisho wa BWANA na utukufu wa enzi yake, atakapoondoka ili aitetemeshe mno dunia.
bali BWANA wa majeshi ametukuzwa katika hukumu, na Mungu aliye Mtakatifu ametakaswa katika haki.
Ole wao wanaostarehe katika Sayuni, na hao wanaokaa salama katika mlima wa Samaria, watu mashuhuri wa taifa lililo la kwanza, ambao nyumba ya Israeli huwaendea.
Basi ningojeeni, asema BWANA, hata siku ile nitakapoondoka kuteka mateka; maana nimeazimia kuwakusanya mataifa, ili nizikutanishe falme, nipate kuwamwagia ghadhabu yangu; naam, ukali wote wa hasira yangu; kwa maana dunia yote itateketezwa kwa moto wa wivu wangu.