Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Zaburi 7:6 - Swahili Revised Union Version

6 BWANA uondoke kwa hasira yako; Ujiinue Juu ya ujeuri wa watesi wangu; Uamke kwa ajili yangu; Umeamuru hukumu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

6 Inuka ee Mwenyezi-Mungu, kwa hasira yako, uikabili ghadhabu ya maadui zangu. Inuka, ee Mungu wangu, wewe umeamuru haki ifanyike.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

6 Inuka ee Mwenyezi-Mungu, kwa hasira yako, uikabili ghadhabu ya maadui zangu. Inuka, ee Mungu wangu, wewe umeamuru haki ifanyike.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

6 Inuka ee Mwenyezi-Mungu, kwa hasira yako, uikabili ghadhabu ya maadui zangu. Inuka, ee Mungu wangu, wewe umeamuru haki ifanyike.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

6 Amka kwa hasira yako, Ee Mwenyezi Mungu, inuka dhidi ya ghadhabu ya adui zangu. Amka, Mungu wangu, uamue haki.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

6 Amka kwa hasira yako, Ee bwana, inuka dhidi ya ghadhabu ya adui zangu. Amka, Mungu wangu, uamue haki.

Tazama sura Nakili




Zaburi 7:6
21 Marejeleo ya Msalaba  

Naye Absalomu na watu wote wa Israeli wakasema, Ushauri wa Hushai, Mwarki, ni mwema kuliko ushauri wa Ahithofeli. Kwa maana BWANA alikuwa amekusudia kuuvunja ushauri mwema wa Ahithofeli, ili BWANA alete mabaya juu ya Absalomu.


BWANA ndiye afanyaye mambo ya haki, Na hukumu kwa wote wanaoonewa.


Kwa ajili ya kuonewa kwao wanyonge, Kwa ajili ya kuugua kwao wahitaji, Sasa nitasimama, asema BWANA, Nitamweka salama yeye wanayemfyonya.


Nijapopitia katika shida, Unanilinda juu ya hasira ya adui zangu, Unaunyosha mkono wako, Na mkono wako wa kulia unaniokoa.


Maana adui ameifuatia nafsi yangu, Ameutupa chini uzima wangu. Amenikalisha mahali penye giza, Kama watu waliokufa zamani.


BWANA, uinuke, Mungu wangu, uniokoe, Maana umewapiga taya adui zangu wote; Umewavunja meno wasio haki.


Ee BWANA, uwapinge hao wanaonipinga, Upigane nao wanaopigana nami.


Uamke, uwe macho ili kunipatia hukumu Kwa ajili ya madai yangu, Mungu wangu na Bwana wangu.


Amka, Bwana, mbona umelala? Ondoka, usitutupe milele.


Uinuke, uwe msaada wetu, Utukomboe kwa ajili ya fadhili zako.


Na Wewe, BWANA, Mungu wa majeshi, Mungu wa Israeli, uinuke. Uwapatilize mataifa yote; Usimrehemu hata mmoja wa wale wapangao maovu kwa hila.


Ee Bwana, wamekuwa kama ndoto wakati wa kuamka, Uondokapo utaidharau sanamu yao.


Upite na kupaona palipoharibika milele; Adui ameufanya kila ubaya katika patakatifu.


Ndipo Bwana alipoamka kama aliyelala usingizi, Kama shujaa apigaye kelele kwa sababu ya mvinyo;


BWANA asimama ili atete, asimama ili awahukumu watu.


Basi, sasa nitasimama; asema BWANA; sasa nitajiinua, sasa nitajitukuza.


Basi sasa, BWANA, Mungu wetu, utuokoe kutoka kwa mkono wake, falme zote za dunia zipate kujua ya kuwa wewe ndiwe BWANA, wewe peke yako.


Amka, amka, jivike nguvu, Ee mkono wa Bwana; Amka kama katika siku zile za kale, Katika vizazi vile vya zamani.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo