Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Isaya 33:11 - Swahili Revised Union Version

11 Ninyi mtachukua mimba ya makapi, mtazaa majani makavu; pumzi yenu ni moto utakaowateketeza wenyewe.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

11 Mipango yenu yote ni kama makapi, na matokeo yake ni takataka tupu. Pumzi yangu itawaangamiza kama moto.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

11 Mipango yenu yote ni kama makapi, na matokeo yake ni takataka tupu. Pumzi yangu itawaangamiza kama moto.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

11 Mipango yenu yote ni kama makapi, na matokeo yake ni takataka tupu. Pumzi yangu itawaangamiza kama moto.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

11 Mlichukua mimba ya makapi, mkazaa mabua; pumzi yenu ni moto unaowateketeza.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

11 Mlichukua mimba ya makapi, mkazaa mabua, pumzi yenu ni moto uwateketezao.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

11 Ninyi mtachukua mimba ya makapi, mtazaa majani makavu; pumzi yenu ni moto utakaowateketeza wenyewe.

Tazama sura Nakili




Isaya 33:11
20 Marejeleo ya Msalaba  

Wao hutunga mimba ya madhara, na kuzaa uovu, Na mioyo yao hutunga udanganyifu.


Mbona mataifa yanafanya ghasia, Na watu kuwaza mambo ya bure?


Tazama, huyu ametunga uovu, Amechukua mimba ya madhara, amezaa uongo.


Amechimba shimo, amelichimba chini sana, Akatumbukia katika handaki aliyoichimba!


Na mtu hodari atakuwa kama makumbi, na kazi yake kama cheche ya moto; nao watawaka pamoja, wala hapana atakayewazima.


Mataifa wananguruma kama ngurumo ya maji mengi; Lakini atawakemea, nao watakimbia mbali sana, Watafukuzwa kama makapi milimani mbele ya upepo, Na kama mavumbi vuruvuru mbele ya tufani.


Tumekuwa na mimba, tumekuwa na uchungu, tumekuwa kana kwamba tumezaa upepo; hatukufanya wokovu wowote duniani, wala hawakuanguka wakaao duniani.


Kwa hiyo kama vile muali wa moto uteketezavyo mabua makavu, na kama manyasi makavu yaangukavyo katika muali wa moto; kadhalika shina lao litakuwa kama ubovu, na ua lao litapeperushwa juu kama mavumbi; kwa sababu wameikataa sheria ya BWANA wa majeshi, na kulidharau neno lake aliye Mtakatifu wa Israeli.


Hakuna anayeshitaki kwa haki, wala hapana atetaye kwa kweli; hutumainia ubatili, hunena uongo; hupata mimba ya madhara, na kuzaa uovu.


Kwa sababu hiyo Bwana hatawafurahia vijana wao, wala hatawahurumia yatima zao wala wajane wao; maana kila mtu ni mnajisi, dhalimu, na kila ulimi hunena upumbavu. Pamoja na hayo yote hasira yake haikugeukia mbali, lakini mkono wake umenyoshwa hata sasa.


Kilipokuwa kwako, hakikuwa mali yako? Na kilipokuwa kimekwisha kuuzwa, thamani yake haikuwa katika uwezo wako? Ilikuwaje hata ukaweka neno hili moyoni mwako? Hukumwambia uongo mwanadamu, bali Mungu.


Halafu ile tamaa ikiisha kuchukua mimba huzaa dhambi, na ile dhambi ikiisha kukomaa huzaa mauti.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo