Isaya 3:3 - Swahili Revised Union Version jemadari aliye juu ya watu hamsini, na mtu mstahifu, na mshauri, na fundi aliye stadi, na mganga ajuaye uganga sana. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema majemadari wa vikosi vya watu hamsini, na watu wenye vyeo, washauri, wachawi stadi na walozi hodari. Biblia Habari Njema - BHND majemadari wa vikosi vya watu hamsini, na watu wenye vyeo, washauri, wachawi stadi na walozi hodari. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza majemadari wa vikosi vya watu hamsini, na watu wenye vyeo, washauri, wachawi stadi na walozi hodari. Neno: Bibilia Takatifu jemadari wa kikosi cha watu hamsini na mtu mwenye cheo, mshauri, fundi stadi na msihiri mjanja. Neno: Maandiko Matakatifu jemadari wa kikosi cha watu hamsini na mtu mwenye cheo, mshauri, fundi stadi na mlozi mjanja. BIBLIA KISWAHILI jemadari aliye juu ya watu hamsini, na mtu mstahifu, na mshauri, na fundi aliye stadi, na mganga ajuaye uganga sana. |
Zaidi ya hayo utajipatia katika watu hawa watu walio na uwezo, wenye kumcha Mungu, watu wa kweli, wenye kuchukia mapato ya udhalimu; ukawaweka juu yao, wawe wakuu wa maelfu, na wakuu wa mamia, na wakuu wa hamsini hamsini, na wakuu wa kumi kumi;
Musa akamwambia BWANA Ee Bwana, mimi si msemaji, tokea zamani, wala tokea hapo uliposema na mtumishi wako; maana mimi si mwepesi wa kusema, na ulimi wangu ni mzito.
Kwa sababu hiyo watu wangu wamechukuliwa mateka, kwa kukosa kuwa na maarifa; na watu wao wenye cheo wana njaa, na wengi wao waona kiu sana.
Basi nikatwaa vichwa vya makabila yenu wenye akili, waliojulikana, nikawafanya wawe vichwa juu yenu, makamanda wa maelfu, na makamanda wa mamia, na makamanda wa hamsini hamsini, na makamanda wa kumi kumi, na wenye amri, kwa kadiri ya makabila yenu.
Ndipo akawaambia hao Zeba na Salmuna, Hao watu mliowaua huko Tabori walikuwa watu wa namna gani? Wakamjibu, Walikuwa kama wewe ulivyo; kila mmoja alikuwa anafanana na wana wa mfalme.
Naye atawaweka kwake kuwa wakuu juu ya maelfu, na makamanda juu ya hamsini hamsini; na wengine atawaweka walime shamba lake, na kuvuna mavuno yake, na kufanyiza zana zake za vita, na vyombo vya magari yake.