Na itakuwa atakayeokoka na upanga wa Hazaeli, Yehu atamwua; na atakayeokoka na upanga wa Yehu, Elisha atamwua.
Isaya 24:17 - Swahili Revised Union Version Hofu, na shimo, na mtego, viko juu yako, Ee mwenye kukaa duniani. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Hofu, mashimo na mitego, hivi ndivyo vinavyowangojeni enyi wakazi wa dunia. Biblia Habari Njema - BHND Hofu, mashimo na mitego, hivi ndivyo vinavyowangojeni enyi wakazi wa dunia. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Hofu, mashimo na mitego, hivi ndivyo vinavyowangojeni enyi wakazi wa dunia. Neno: Bibilia Takatifu Hofu, shimo na mtego vinakungojea, ewe mtu ukaaye duniani. Neno: Maandiko Matakatifu Hofu, shimo na mtego vinakungojea, ewe mtu ukaaye duniani. BIBLIA KISWAHILI Hofu, na shimo, na mtego, viko juu yako, Ee mwenye kukaa duniani. |
Na itakuwa atakayeokoka na upanga wa Hazaeli, Yehu atamwua; na atakayeokoka na upanga wa Yehu, Elisha atamwua.
Naye atakuwa ni mahali patakatifu; bali ni jiwe la kujikwaza na mwamba wa kujikwaa kwa nyumba za Israeli zote mbili, na mtego na tanzi kwa wenyeji wa Yerusalemu.
Basi, BWANA asema hivi, Tazama, nitaleta mabaya juu yao, ambayo hawataweza kuyakimbia; nao watanililia, lakini sitawasikiliza.
Na kufa kutachaguliwa kuliko kuishi na mabaki wote waliosalia katika jamaa hii mbovu, waliosalia kila mahali nilikowafukuza, asema BWANA wa majeshi.
Umeziita kama katika siku ya mkutano wa makini; Hofu zangu zije pande zote; Wala hapana hata mmoja aliyepona wala kusalia Katika siku ya hasira ya BWANA; Hao niliowabeba na kuwalea Huyo adui yangu amewakomesha.
Tena wavu wangu nitautandika juu yake, naye atanaswa kwa mtego wangu; nami nitampeleka Babeli, mpaka nchi ya Wakaldayo; lakini hataiona, ingawa atakufa huko.
Maana Bwana MUNGU asema hivi; Je! U zaidi sana nitakapoleta hukumu zangu nne zilizo kali juu ya Yerusalemu, yaani, upanga, na njaa, na wanyama wabaya, na tauni, niwakatilie mbali nayo wanadamu na wanyama?
Ni kama mtu aliyemkimbia simba, akakutana na dubu; au aliingia katika nyumba akauegemeza mkono wake ukutani, nyoka akamwuma.