Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

Maombolezo 2:22 - Swahili Revised Union Version

22 Umeziita kama katika siku ya mkutano wa makini; Hofu zangu zije pande zote; Wala hapana hata mmoja aliyepona wala kusalia Katika siku ya hasira ya BWANA; Hao niliowabeba na kuwalea Huyo adui yangu amewakomesha.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

22 Umewaalika kama kwenye sikukuu maadui zangu walionitisha kila upande. Katika siku ya hasira yako ee Mwenyezi-Mungu, hakuna aliyetoroka au kunusurika. Wale niliowazaa na kuwalea adui zangu wamewaangamiza.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

22 Umewaalika kama kwenye sikukuu maadui zangu walionitisha kila upande. Katika siku ya hasira yako ee Mwenyezi-Mungu, hakuna aliyetoroka au kunusurika. Wale niliowazaa na kuwalea adui zangu wamewaangamiza.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

22 Umewaalika kama kwenye sikukuu maadui zangu walionitisha kila upande. Katika siku ya hasira yako ee Mwenyezi-Mungu, hakuna aliyetoroka au kunusurika. Wale niliowazaa na kuwalea adui zangu wamewaangamiza.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

22 “Kama ulivyoita siku ya karamu, ndivyo ulivyoagiza mapigo dhidi yangu kila upande. Katika siku ya hasira ya Mwenyezi Mungu hakuna yeyote aliyekwepa au kupona; wale niliowatunza na kuwalea, adui yangu amewaangamiza.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

22 “Kama ulivyoita siku ya karamu, ndivyo ulivyoagiza hofu kuu dhidi yangu kila upande. Katika siku ya hasira ya bwana hakuna yeyote aliyekwepa au kupona; wale niliowatunza na kuwalea, adui yangu amewaangamiza.”

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

22 Umeziita kama katika siku ya mkutano wa makini; Hofu zangu zije pande zote; Wala hapana hata mmoja aliyepona wala kusalia Katika siku ya hasira ya BWANA; Hao niliowabeba na kuwalea Huyo adui yangu amewakomesha.

Tazama sura Nakili

Maombolezo 2:22
16 Marejeleo ya Msalaba  

Kwa hiyo akaleta juu yao mfalme wa Wakaldayo, aliyewaua vijana wao kwa upanga nyumbani mwa patakatifu pao, asiwahurumie kijana wala mwanamwali, mzee wala mnyonge; akawatia wote mkononi mwake.

Maana nimesikia wengi wakinong'onezana; Hofu katika pande zote. Waliposhauriana juu yangu, Walipanga kunitoa uhai wangu.

Kila wakati litakapopita litawachukueni. Maana litapita asubuhi baada ya asubuhi, wakati wa mchana na wakati wa usiku; na kuifahamu habari ile kutakuwa kitisho tu.

Basi, BWANA asema hivi, Tazama, nitaleta mabaya juu yao, ambayo hawataweza kuyakimbia; nao watanililia, lakini sitawasikiliza.

Je! Umemkataa Yuda kabisa? Roho yako imeichukia Sayuni? Mbona umetupiga, tusiwe na dawa ya kutuponya? Tulitazamia amani, lakini hayakuja mema yoyote, tulitazamia wakati wa kupona, na tazama, kufadhaika tu!

Hata ikawa, asubuhi, Pashuri huyo akamtoa Yeremia katika mkatale. Ndipo Yeremia akamwambia, BWANA hakukuita jina lako Pashuri, bali Magor-misabibu.

Na baada ya hayo, asema BWANA, nitamtia Sedekia, mfalme wa Yuda, na watumishi wake, na watu wote waliosalia ndani ya mji huu, baada ya tauni ile, na upanga, na njaa, katika mkono wa Nebukadneza, mfalme wa Babeli, na katika mikono ya adui zao, na katika mikono ya watu wale wanaowatafuta roho zao; naye atawaua kwa ukali wa upanga; hatawaachilia, wala hatawahurumia, wala hatawarehemu.

Basi, sasa, BWANA, Mungu wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Kwa nini mnafanya uovu huu mkubwa juu ya nafsi zenu wenyewe, kujikatilia mbali mwanamume na mwanamke, mtoto mchanga na anyonyaye, mtoke kati ya Yuda, msijiachie mtu abakiye;

Nimeyaona haya kwa sababu gani? Wamefadhaika, wamerudi nyuma; mashujaa wao wamevunjikavunjika; wanakimbia upesi sana, hawatazami nyuma; hofu iko pande zote; asema BWANA.

Msitoke kwenda mashambani, wala msitembee njiani, kwa maana upanga wa adui uko huko; hofu ziko pande zote.

Utalaaniwa uzao wa tumbo lako, na uzao wa nchi yako, kuongezeka kwa ng'ombe wako, na wadogo wa kondoo wako.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo