Kama BWANA wa majeshi asingalituachia mabaki machache sana, tungalikuwa kama Sodoma, tungalifanana na Gomora.
Isaya 24:13 - Swahili Revised Union Version Maana katikati ya dunia, katikati ya mataifa, itakuwa hivi; kama wakati utikiswapo mzeituni, kama wakati waokotapo zabibu baada ya mavuno yake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kama vile zeituni chache tu juu ya mzeituni au tini chache tu juu ya mtini baada ya kumaliza mavuno, ndivyo itakavyokuwa katika nchi zote: Watu wachache watabakia hai. Biblia Habari Njema - BHND Kama vile zeituni chache tu juu ya mzeituni au tini chache tu juu ya mtini baada ya kumaliza mavuno, ndivyo itakavyokuwa katika nchi zote: Watu wachache watabakia hai. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kama vile zeituni chache tu juu ya mzeituni au tini chache tu juu ya mtini baada ya kumaliza mavuno, ndivyo itakavyokuwa katika nchi zote: watu wachache watabakia hai. Neno: Bibilia Takatifu Ndivyo itakavyokuwa duniani na miongoni mwa mataifa, kama vile wakati mzeituni upigwavyo, au kama vile wakati masazo yabakiavyo baada ya zabibu kuvunwa. Neno: Maandiko Matakatifu Ndivyo itakavyokuwa duniani na miongoni mwa mataifa, kama vile wakati mzeituni upigwavyo, au kama vile wakati masazo yabakiavyo baada ya zabibu kuvunwa. BIBLIA KISWAHILI Maana katikati ya dunia, katikati ya mataifa, itakuwa hivi; kama wakati utikiswapo mzeituni, kama wakati waokotapo zabibu baada ya mavuno yake. |
Kama BWANA wa majeshi asingalituachia mabaki machache sana, tungalikuwa kama Sodoma, tungalifanana na Gomora.
Tena itakuwa katika siku hiyo, utukufu wa Yakobo utapungua na kunona kwa mwili wake kutakwisha.
Tena itakuwa katika siku hiyo, BWANA atayapigapiga matunda yake toka gharika ya Mto hadi kijito cha Misri, nanyi mtakusanywa mmoja mmoja, enyi wana wa Israeli.
Na ijapokuwa imebaki sehemu moja katika sehemu kumi ndani yake, italiwa hii nayo; kama mvinje na kama mwaloni, ambao shina lake limebaki, ingawa imekatwa; kadhalika mbegu takatifu ndiyo shina lake.
Nao watakaoukimbia upanga, watatoka katika nchi ya Misri, na kuiingia katika nchi ya Yuda, watu wachache sana; na wote wa Yuda waliosalia, waliokwenda katika nchi ya Misri ili kukaa huko, watajua ni neno la nani litakalosimama, neno langu, au neno lao.
Lakini watakaokimbia watakimbia, nao watakuwa juu ya milima kama hua wa bondeni, wote wakilia, kila mmoja katika uovu wake.
Na mtakapovuna mavuno ya nchi yenu, usivune kabisa katika pembe za shamba lako, wala usiyakusanye masazo ya mavuno yako;
Hakika nitakukusanya, Ee Yakobo, nyote pia; Bila shaka nitawakusanya waliobaki wa Israeli; Nitawaweka pamoja kama kondoo katika zizi; Kama kundi la kondoo katika malisho yao; Watafanya mvumo kwa wingi wa watu;
Ole wangu! Maana mimi ni kama hapo walipokwisha kuyachuma matunda ya wakati wa joto, kama zabibu zichumwazo baada ya mavuno; hapana shada la kuliwa; roho yangu inatamani tini iivayo kwanza.
Na kama siku hizo zisingalifupishwa, asingeokoka mtu yeyote; lakini kwa ajili ya wateule siku hizo zitafupishwa.
Lakini unayo majina machache katika Sardi, watu wasioyatia mavazi yao uchafu. Nao watakwenda pamoja nami hali wamevaa mavazi meupe, kwa kuwa wamestahili.