Isaya 22:14 - Swahili Revised Union Version Na yeye BWANA wa majeshi akafunua haya masikioni mwangu, Ni kweli, uovu huu hautatakaswa wala kuwatokeni hata mfe; asema Bwana, BWANA wa majeshi. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mwenyezi-Mungu wa majeshi alinifunulia haya akisema: “Hakika hawatasamehewa uovu huu, watakufa bila kusamehewa. Mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi nimesema.” Biblia Habari Njema - BHND Mwenyezi-Mungu wa majeshi alinifunulia haya akisema: “Hakika hawatasamehewa uovu huu, watakufa bila kusamehewa. Mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi nimesema.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mwenyezi-Mungu wa majeshi alinifunulia haya akisema: “Hakika hawatasamehewa uovu huu, watakufa bila kusamehewa. Mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi nimesema.” Neno: Bibilia Takatifu Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni amelifunua hili nikiwa ninasikia: Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, asema: “Hadi siku ya kufa kwenu, dhambi hii haitafanyiwa upatanisho.” Neno: Maandiko Matakatifu bwana Mwenye Nguvu Zote amelifunua hili nikiwa ninasikia: Bwana, bwana Mwenye Nguvu Zote, asema: “Mpaka siku ya kufa kwenu, dhambi hii haitafanyiwa upatanisho.” BIBLIA KISWAHILI Na yeye BWANA wa majeshi akafunua haya masikioni mwangu, Ni kweli, uovu huu hautatakaswa wala kuwatokeni hata mfe; asema Bwana, BWANA wa majeshi. |
Nami nitaadhibu ulimwengu kwa sababu ya ubaya wake, na wenye dhambi kwa sababu ya hatia yao; nami nitaikomesha fahari yao wenye kiburi; nami nitayashusha chini majivuno yao walio wakali;
Kwa maana, tazama, BWANA anakuja kutoka mahali pake, ili kuwaadhibu wakaao duniani, kwa sababu ya uovu wao; ardhi nayo itafunua damu yake, wala haitawafunika tena watu wake waliouawa.
basi, uovu huu utakuwa kwenu kama mahali palipobomoka, kuanguka patokezapo katika ukuta mrefu, ambapo kuvunjika kwake huja ghafla kwa mara moja.
Lakini yeye naye ana akili, naye ataleta uovu, wala hatayatangua maneno yake; bali ataondoka juu ya nyumba yao watendao mabaya, na juu ya msaada wa hao watendao maovu.
BWANA wa majeshi asema katika masikio yangu, Hakika majumba mengi yatakuwa ukiwa, naam, majumba makubwa, mazuri, yatakuwa hayana watu.
Hatakuwapo tena mtoto wa siku chache, wala mzee asiyetimia siku zake; kwa maana mtoto atakufa mwenye umri wa miaka mia; bali mtenda dhambi mwenye umri wa miaka mia atalaaniwa.
maovu yenu na maovu ya baba zenu pamoja, asema BWANA, ninyi mliofukiza uvumba juu ya milima, na kunitukana juu ya vilima; basi, kwa ajili ya hayo nitawapimia kwanza kazi yao vifuani mwao.
Katika uchafu wako mna uasherati, kwa maana nimekusafisha, ila wewe hukusafika; hutasafishwa tena uchafu wako ukutoke, hadi nitakapokuwa nimeituliza hasira yangu kwako.
Hakika Bwana MUNGU hatafanya neno lolote, bila kuwafunulia watumishi wake manabii siri yake.
Na kwa hiyo nimeapa juu ya nyumba ya Eli, ya kwamba uovu wa nyumba ya Eli hautasafika kwa dhabihu wala kwa sadaka hata milele.