Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

Isaya 26:21 - Swahili Revised Union Version

21 Kwa maana, tazama, BWANA anakuja kutoka mahali pake, ili kuwaadhibu wakaao duniani, kwa sababu ya uovu wao; ardhi nayo itafunua damu yake, wala haitawafunika tena watu wake waliouawa.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

21 Maana Mwenyezi-Mungu aja kutoka kwake juu, kutoka makao yake huko mbinguni; kuwaadhibu wakazi wa dunia kwa uovu wao. Nayo dunia haitaficha tena wale waliouawa, ila itaufichua umwagaji damu wote.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

21 Maana Mwenyezi-Mungu aja kutoka kwake juu, kutoka makao yake huko mbinguni; kuwaadhibu wakazi wa dunia kwa uovu wao. Nayo dunia haitaficha tena wale waliouawa, ila itaufichua umwagaji damu wote.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

21 Maana Mwenyezi-Mungu aja kutoka kwake juu, kutoka makao yake huko mbinguni; kuwaadhibu wakazi wa dunia kwa uovu wao. Nayo dunia haitaficha tena wale waliouawa, ila itaufichua umwagaji damu wote.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

21 Tazama, Mwenyezi Mungu anakuja kutoka makao yake ili kuwaadhibu watu wa dunia kwa ajili ya dhambi zao. Dunia itadhihirisha umwagaji damu juu yake, wala haitaendelea kuwaficha watu wake waliouawa.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

21 Tazama, bwana anakuja kutoka makao yake ili kuwaadhibu watu wa dunia kwa ajili ya dhambi zao. Dunia itadhihirisha umwagaji damu juu yake, wala haitaendelea kuwaficha watu wake waliouawa.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

21 Kwa maana, tazama, BWANA anakuja kutoka mahali pake, ili kuwaadhibu wakaao duniani, kwa sababu ya uovu wao; ardhi nayo itafunua damu yake, wala haitawafunika tena watu wake waliouawa.

Tazama sura Nakili

Isaya 26:21
28 Marejeleo ya Msalaba  

Ee nchi, usiifunike damu yangu, Na kilio changu kisipate mahali pa kupumzika.

Mbingu zitafunua wazi uovu wake, Nayo nchi itainuka kinyume chake.

Nanyi mtafanya nini siku ya kujiliwa, na wakati wa uangamivu, utakaokuja kutoka mbali sana? Je! Mtamkimbilia nani mpate msaada? Na utukufu wenu mtauacha wapi?

Nami nitaadhibu ulimwengu kwa sababu ya ubaya wake, na wenye dhambi kwa sababu ya hatia yao; nami nitaikomesha fahari yao wenye kiburi; nami nitayashusha chini majivuno yao walio wakali;

Maana BWANA ameniambia hivi, Mimi nitatulia, na kuangalia katika makazi yangu, kama wakati wa mwangaza mweupe wa jua kali, mfano wa wingu la umande katika joto la mavuno.

Na yeye BWANA wa majeshi akafunua haya masikioni mwangu, Ni kweli, uovu huu hautatakaswa wala kuwatokeni hata mfe; asema Bwana, BWANA wa majeshi.

Naye atajiliwa na BWANA wa majeshi kwa ngurumo, na tetemeko la nchi, na sauti kuu, na chamchela, na tufani, na mwali wa moto uteketezao.

Tazama, neno hili limeandikwa mbele zangu. Sitanyamaza, lakini nitalipa, naam, mimi nitawalipa ujira wao vifuani mwao;

maovu yenu na maovu ya baba zenu pamoja, asema BWANA, ninyi mliofukiza uvumba juu ya milima, na kunitukana juu ya vilima; basi, kwa ajili ya hayo nitawapimia kwanza kazi yao vifuani mwao.

Sauti ya fujo itokayo mjini! Sauti itokayo hekaluni! Sauti ya BWANA awalipaye adui zake adhabu!

Akaniambia, Mwanadamu, je! Unayaona wanayoyafanya, yaani, haya machukizo makubwa wanayoyafanya nyumba ya Israeli hapa, ili niende zangu mbali na patakatifu pangu? Lakini utaona tena machukizo makubwa mengine.

Enyi wapumbavu; aliyevifanya vya nje, siye yeye aliyevifanya vya ndani pia?

ili kwa kizazi hiki itakwe damu ya manabii wote, iliyomwagika tangu kupigwa msingi wa ulimwengu;

kwa kuwa walimwaga damu ya watakatifu na ya manabii, nawe umewapa damu wainywe; ndiyo wanayostahili.

Na ndani yake ilionekana damu ya manabii, na ya watakatifu, na ya wale wote waliouawa juu ya nchi.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo