Isaya 13:3 - Swahili Revised Union Version Mimi mwenyewe nimewaamuru watu wangu waliowekwa wakfu kwangu, naam, nimewaita watu wangu walio hodari kwa ajili ya hasira yangu, watu wangu wenye kiburi. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mimi nimewaamuru wateule wangu, nimewaita mashujaa wangu, hao wenye kunitukuza wakishangilia, waje kutekeleza lengo la hasira yangu.” Biblia Habari Njema - BHND Mimi nimewaamuru wateule wangu, nimewaita mashujaa wangu, hao wenye kunitukuza wakishangilia, waje kutekeleza lengo la hasira yangu.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mimi nimewaamuru wateule wangu, nimewaita mashujaa wangu, hao wenye kunitukuza wakishangilia, waje kutekeleza lengo la hasira yangu.” Neno: Bibilia Takatifu Nimewaamuru watakatifu wangu; nimewaita mashujaa wangu waitimize hasira yangu: wale wanaoshangilia ushindi wangu. Neno: Maandiko Matakatifu Nimewaamuru watakatifu wangu; nimewaita mashujaa wangu waitimize hasira yangu: wale wanaoshangilia ushindi wangu. BIBLIA KISWAHILI Mimi mwenyewe nimewaamuru watu wangu waliowekwa wakfu kwangu, naam, nimewaita watu wangu walio hodari kwa ajili ya hasira yangu, watu wangu wenye kiburi. |
Amenyosha mkono wake juu ya bahari, amezitikisa falme; Bwana ametoa amri katika habari za Kanaani, kuziangamiza ngome zake.
Naye atawatolea ishara mataifa toka mbali, Naye atawapigia miruzi tokea mwisho wa nchi; Na tazama, watakuja mbio mbio upesi sana.
angalieni, nitatuma watu na kuzitwaa jamaa zote za upande wa kaskazini, asema BWANA, nami nitatuma ujumbe kwa Nebukadneza, mfalme wa Babeli, mtumishi wangu, nami nitawaleta juu ya nchi hii, na juu yao wakaao ndani yake, na juu ya mataifa haya yote yaliyoko pande zote; nami nitawaangamiza kabisa, na kuwafanya kitu cha kushangaza, na kitu cha kuzomewa, na ukiwa wa daima.
Wala isizimie mioyo yenu, wala msiiogope habari itakayosikiwa katika nchi; maana habari itakuja mwaka mmoja, na baadaye mwaka wa pili habari itakuja, na udhalimu katika nchi, mwenye kutawala akishindana na mwenye kutawala.
Babeli ujapopanda mbinguni, na ujapopafanya mahali pa juu penye nguvu zake kuwa ngome, hata hivyo toka kwangu wenye kuangamiza watamwendea, asema BWANA.
Fanyeni haraka, mje, enyi mataifa yote, wa pande zote, jikusanyeni pamoja; na huko wateremshe mashujaa wako wote, Ee BWANA.
Nyamaza kimya mbele za Bwana MUNGU; Kwa maana siku ya BWANA iko karibu; Kwa kuwa BWANA ametayarisha dhabihu, Amewatakasa wageni wake.
Furahini juu yake, enyi mbingu, na enyi watakatifu, mitume na manabii; kwa maana Mungu ametoa hukumu kwa ajili yenu juu yake.