Mbona mnataka kupigwa, hata sasa, hata mkazidi kuasi? Kichwa chote ni kigonjwa, moyo wote umezimia.
Hosea 5:2 - Swahili Revised Union Version Nao walioasi wameongeza sana ufisadi wao; lakini mimi ndiye awakaripiaye wote pia. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mmechimba shimo refu la kuwanasa huko Shitimu. Lakini mimi nitawaadhibuni nyote. Biblia Habari Njema - BHND Mmechimba shimo refu la kuwanasa huko Shitimu. Lakini mimi nitawaadhibuni nyote. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mmechimba shimo refu la kuwanasa huko Shitimu. Lakini mimi nitawaadhibuni nyote. Neno: Bibilia Takatifu Waasi wamezidisha sana mauaji. Mimi nitawatiisha wote. Neno: Maandiko Matakatifu Waasi wamezidisha sana mauaji. Mimi nitawatiisha wote. BIBLIA KISWAHILI Nao walioasi wameongeza sana ufisadi wao; lakini mimi ndiye awakaripiaye wote pia. |
Mbona mnataka kupigwa, hata sasa, hata mkazidi kuasi? Kichwa chote ni kigonjwa, moyo wote umezimia.
Ole wao wanaojitahidi kumficha BWANA mashauri yao, na matendo yao yamo gizani, nao husema, Ni nani atuonaye? Nani atujuaye?
Hapo ndipo waliposema, Njooni na tufanye mashauri juu ya Yeremia; maana sheria haitampotea kuhani, wala shauri halitampotea mwenye hekima, wala neno halitampotea nabii. Njooni, na tumpige kwa ndimi zetu, wala tusiyaangalie maneno yake yoyote.
Ee BWANA, macho yako je! Hayaangalii uaminifu? Umewapiga, lakini hawakuhuzunika; umewakomesha, lakini wamekataa kurudiwa wamefanya nyuso zao kuwa ngumu kuliko mwamba wamekataa kurudi.
Ni waasi kupita kiasi wote pia, waendao huku na huko wakisingizia, ni shaba na chuma hao, hutenda dhuluma wote pia.
Hapana neno ila kuapa kwa uongo, na kuvunja ahadi, na kuua, na kuiba, na kuzini; huruka mpaka, na kumwaga damu mfululizo.
Kwa sababu hiyo nimewakatakata kwa vinywa vya manabii; nimewaua kwa maneno ya kinywa changu; na hukumu yangu itatokea kama mwanga.
Na kama vile makundi ya wanyang'anyi wamwoteavyo mtu, ndivyo kundi la makuhani wauavyo katika njia ielekeayo Shekemu; naam, wametenda mambo maovu sana.
Uovu wao wote u katika Gilgali; maana huko niliwachukia; kwa sababu ya uovu wa matendo yao nitawafukuza watoke katika nyumba yangu; sitawapenda tena; wakuu wao wote ni waasi.