Kwa maana watatahayarika kwa sababu ya mialoni mliyoitamani, nanyi mtaaibishwa kwa sababu ya bustani mlizozichagua.
Hosea 4:19 - Swahili Revised Union Version Upepo umemfunika kwa mbawa zake; nao watatahayarika kwa sababu ya dhabihu zao. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Basi, kimbunga kitawapeperusha, na watayaonea aibu matambiko yao kwa miungu ya uongo. Biblia Habari Njema - BHND Basi, kimbunga kitawapeperusha, na watayaonea aibu matambiko yao kwa miungu ya uongo. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Basi, kimbunga kitawapeperusha, na watayaonea aibu matambiko yao kwa miungu ya uongo. Neno: Bibilia Takatifu Kisulisuli kitawafagilia mbali na dhabihu zao zitawaletea aibu. Neno: Maandiko Matakatifu Kisulisuli kitawafagilia mbali na dhabihu zao zitawaletea aibu. BIBLIA KISWAHILI Upepo umemfunika kwa mbawa zake; nao watatahayarika kwa sababu ya dhabihu zao. |
Kwa maana watatahayarika kwa sababu ya mialoni mliyoitamani, nanyi mtaaibishwa kwa sababu ya bustani mlizozichagua.
Watarudishwa nyuma, wataaibishwa sana, hao wanaotumainia sanamu za mawe, na kuziambia sanamu za madini, Ninyi ndinyi miungu yetu.
Ee BWANA, tumaini la Israeli, wote wakuachao watatahayarika. Wao watakaojitenga nami wataandikwa katika mchanga, kwa sababu wamemwacha BWANA, kisima cha maji yaliyo hai.
BWANA asema hivi, Angalia, nitaamsha juu ya Babeli, na juu yao wakaao Leb-kamai, upepo uharibuo.
Wakati nitakapopenda nitawaadhibu; na hao mataifa watakusanyika juu yao, watakapofungwa kwa sababu ya makosa yao mawili.
Nayo itachukuliwa Ashuru, iwe zawadi kwa mfalme Yarebu; Efraimu atapata aibu, na Israeli atalionea haya shauri lake mwenyewe.
Efraimu hujilisha upepo, na kuandamana na upepo wa mashariki; haachi kuongeza uongo na uharibifu; nao wafanya agano na Ashuru, na mafuta huchukuliwa kwenda Misri.
Ajapokuwa yeye ni mwenye kuzaa sana kati ya ndugu zake, upepo wa mashariki utakuja, hiyo pumzi ya BWANA itokayo upande wa nyikani, na kijito chake cha maji kitakauka, na chemchemi yake itakaushwa; yeye atateka nyara hazina ya vyombo vyote vipendezavyo.