Biblia ya mtandaoni

Matangazo

Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya

Hesabu 9:7 - Swahili Revised Union Version

Sisi tuko katika hali ya unajisi kwa ajili ya maiti wa mtu; nasi tumezuiwa kwa nini hata tusipate kumtolea BWANA matoleo kwa wakati wake ulioagizwa, kati ya wana wa Israeli?

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

wakawaambia, “Sisi tu najisi kwa kuwa tumegusa maiti, lakini kwa nini tukatazwe kumtolea Mwenyezi-Mungu sadaka zake kwa wakati uliopangwa pamoja na Waisraeli wengine?”

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

wakawaambia, “Sisi tu najisi kwa kuwa tumegusa maiti, lakini kwa nini tukatazwe kumtolea Mwenyezi-Mungu sadaka zake kwa wakati uliopangwa pamoja na Waisraeli wengine?”

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

wakawaambia, “Sisi tu najisi kwa kuwa tumegusa maiti, lakini kwa nini tukatazwe kumtolea Mwenyezi-Mungu sadaka zake kwa wakati uliopangwa pamoja na Waisraeli wengine?”

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

wakamwambia Musa, “Tumekuwa najisi kwa sababu tumegusa maiti, lakini kwa nini tuzuiliwe kumtolea Mwenyezi Mungu sadaka yake pamoja na Waisraeli wengine katika wakati ulioamriwa?”

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

wakamwambia Musa, “Tumekuwa najisi kwa sababu tumegusa maiti, lakini kwa nini tuzuiliwe kumtolea bwana sadaka yake pamoja na Waisraeli wengine katika wakati ulioamriwa?”

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Sisi tuko katika hali ya unajisi kwa ajili ya maiti wa mtu; nasi tumezuiwa kwa nini hata tusipate kumtolea BWANA matoleo kwa wakati wake ulioagizwa, kati ya wana wa Israeli?

Tazama sura
Tafsiri zingine

Hesabu 9:7
7 Marejeleo ya Msalaba  

Ndipo mtawaambia, Ni dhabihu ya Pasaka ya BWANA, kwa kuwa alipita juu ya nyumba za wana wa Israeli huko Misri, hapo alipowapiga Wamisri, akaziokoa nyumba zetu. Hao watu wakainamisha vichwa na kusujudia.

Tena, wana wa Israeli na waadhimishe sikukuu ya Pasaka kwa wakati wake ulioagizwa.

Basi walikuwako wanaume kadhaa waliokuwa na unajisi kwa ajili ya maiti wa mtu, hata wasiweze kuishika Pasaka siku hiyo; nao wakaenda mbele ya Musa na Haruni, siku hiyo hao watu wakamwambia,

Musa akawaambia, Ngojeni hapo; hata nipate sikiza BWANA atakaloagiza juu yenu.

Nawe umchinjie Pasaka BWANA, Mungu wako, katika kundi la kondoo na la ng'ombe, mahali atakapochagua BWANA apakalishe jina lake.