Hesabu 6:26 - Swahili Revised Union Version BWANA akuinulie uso wake, na kukupa amani. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mwenyezi-Mungu awaoneshe wema wake na kuwapa amani.’ Biblia Habari Njema - BHND Mwenyezi-Mungu awaoneshe wema wake na kuwapa amani.’ Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mwenyezi-Mungu awaoneshe wema wake na kuwapa amani.’ Neno: Bibilia Takatifu Mwenyezi Mungu akugeuzie uso wake na kukupa amani.” ’ Neno: Maandiko Matakatifu bwana akugeuzie uso wake na kukupa amani.” ’ BIBLIA KISWAHILI BWANA akuinulie uso wake, na kukupa amani. |
Umwangalie sana mtu mkamilifu, Umtazame mtu mnyofu, Maana mwisho wake mtu huyo ni amani.
Nafsi yangu, kwa nini kuinama, Na kufadhaika ndani yangu? Umtumainie Mungu; Kwa maana nitakuja kumsifu, Aliye afya ya uso wangu, Na Mungu wangu.
Maana hawakuitwaa nchi kwa upanga wao, Wala hawakupata ushindi kwa mkono wao; Bali mkono wako wa kulia, naam, mkono wako, Na nuru ya uso wako, kwa kuwa ulipendezwa nao.
Utamlinda yeye ambaye moyo wake umekutegemea Katika amani kamilifu, kwa kuwa anakutumaini.
Mimi nayaumba matunda ya midomo; Amani, amani, kwake yeye aliye mbali, na kwake yeye aliye karibu; asema BWANA; nami nitamponya.
Na mtu huyu atakuwa amani yetu; wakati Mwashuri atakapoingia katika nchi yetu, na kuyakanyaga majumba yetu, hapo mtawaleta wachungaji saba juu yake, na wakuu wanane.
Amani nawaachieni; amani yangu nawapa; niwapavyo mimi sivyo kama ulimwengu utoavyo. Msifadhaike mioyoni mwenu, wala msiwe na woga.
Hayo nimewaambieni mpate kuwa na amani ndani yangu. Ulimwenguni mnayo dhiki; lakini jipeni moyo; mimi nimeushinda ulimwengu.
Basi Yesu akawaambia tena, Amani iwe kwenu; kama Baba alivyonituma mimi, mimi nami nawatuma ninyi.
Basi, baada ya siku nane, wanafunzi wake walikuwamo ndani tena, na Tomaso pamoja nao. Akaja Yesu, na milango imefungwa, akasimama katikati, akasema, Amani iwe kwenu.
Neno lile alilowapelekea wana wa Israeli akihubiri Habari Njema ya amani kwa Yesu Kristo (ndiye Bwana wa wote),
Basi Mungu wa tumaini na awajaze ninyi furaha yote na amani katika kuamini, mpate kuzidi sana kuwa na tumaini, katika nguvu za Roho Mtakatifu.
Basi tukiisha kuhesabiwa haki itokayo katika imani, na muwe na amani kwa Mungu, kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo,
Amani na iwe kwa ndugu, na upendo, pamoja na imani, zitokazo kwa Mungu Baba na kwa Bwana Yesu Kristo.
Na amani ya Mungu, ipitayo akili zote, itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu.
Sasa, Bwana wa amani mwenyewe na awape amani daima kwa njia zote. Bwana awe pamoja nanyi nyote.