Hesabu 5:6 - Swahili Revised Union Version Uwaambie wana wa Israeli, Mtu mume au mke atakapofanya dhambi yoyote, ifanywayo na binadamu, kumwasi BWANA, na mtu huyo akawa na hatia; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Waambie Waisraeli kuwa: Mtu yeyote, mwanamume au mwanamke akitenda dhambi dhidi ya mtu, akakosa uaminifu kwa Mwenyezi-Mungu, mtu huyo ana hatia; Biblia Habari Njema - BHND “Waambie Waisraeli kuwa: Mtu yeyote, mwanamume au mwanamke akitenda dhambi dhidi ya mtu, akakosa uaminifu kwa Mwenyezi-Mungu, mtu huyo ana hatia; Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Waambie Waisraeli kuwa: Mtu yeyote, mwanamume au mwanamke akitenda dhambi dhidi ya mtu, akakosa uaminifu kwa Mwenyezi-Mungu, mtu huyo ana hatia; Neno: Bibilia Takatifu “Waambie Waisraeli, ‘Mwanaume au mwanamke akimkosea mwenzake kwa njia yoyote, na kwa hivyo akawa si mwaminifu kwa Mwenyezi Mungu, mtu huyo ana hatia, Neno: Maandiko Matakatifu “Waambie Waisraeli, ‘Wakati mwanaume au mwanamke akimkosea mwenzake kwa njia yoyote, na kwa hivyo akawa si mwaminifu kwa bwana, mtu huyo ana hatia, BIBLIA KISWAHILI Uwaambie wana wa Israeli, Mtu mume au mke atakapofanya dhambi yoyote, ifanywayo na binadamu, kumwasi BWANA, na mtu huyo akawa na hatia; |
Lakini asipomweza mwana-kondoo, ndipo atakapomletea BWANA hua wawili, au makinda mawili ya njiwa, kuwa ni sadaka yake ya hatia ya jambo hilo alilolikosa; mmoja wa hao ndege kwa sadaka ya dhambi, na wa pili kwa sadaka ya kuteketezwa.
Nao wakawafikia hao wana wa Reubeni, na wana wa Gadi, na hiyo nusu ya kabila la Manase, katika nchi ya Gileadi, na wakasema nao, wakinena,
Yoshua akamwambia Akani, Mwanangu, nakusihi, umtukuze BWANA, Mungu wa Israeli, ukaungame kwake; uniambie sasa ulilolitenda; usinifiche.