Uzia mfalme akawa na ukoma hadi siku ya kufa kwake, akakaa katika nyumba ya pekee, kwa kuwa ni mwenye ukoma; maana alitengwa na nyumba ya BWANA; na Yothamu mwanawe alikuwa kiongozi wa nyumba ya mfalme, akiwatawala watu wa nchi.
Hesabu 5:4 - Swahili Revised Union Version Wana wa Israeli wakafanya hivyo, wakawatoa na kuwaweka nje ya kambi; kama BWANA alivyonena na Musa, ndivyo walivyofanya wana wa Israeli. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Waisraeli walifanya hivyo, wakawafukuza nje ya kambi. Kama Mwenyezi-Mungu alivyomwambia Mose, ndivyo Waisraeli walivyofanya. Biblia Habari Njema - BHND Waisraeli walifanya hivyo, wakawafukuza nje ya kambi. Kama Mwenyezi-Mungu alivyomwambia Mose, ndivyo Waisraeli walivyofanya. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Waisraeli walifanya hivyo, wakawafukuza nje ya kambi. Kama Mwenyezi-Mungu alivyomwambia Mose, ndivyo Waisraeli walivyofanya. Neno: Bibilia Takatifu Waisraeli wakafanya hivyo; wakawatoa nje ya kambi. Wakafanya kama vile Mwenyezi Mungu alivyokuwa amemwelekeza Musa. Neno: Maandiko Matakatifu Waisraeli wakafanya hivyo; wakawatoa nje ya kambi. Wakafanya kama vile bwana alivyokuwa amemwelekeza Musa. BIBLIA KISWAHILI Wana wa Israeli wakafanya hivyo, wakawatoa na kuwaweka nje ya kambi; kama BWANA alivyonena na Musa, ndivyo walivyofanya wana wa Israeli. |
Uzia mfalme akawa na ukoma hadi siku ya kufa kwake, akakaa katika nyumba ya pekee, kwa kuwa ni mwenye ukoma; maana alitengwa na nyumba ya BWANA; na Yothamu mwanawe alikuwa kiongozi wa nyumba ya mfalme, akiwatawala watu wa nchi.
Basi wana wa Israeli wakaenda na kufanya mambo hayo; vile vile kama BWANA alivyowaamuru Musa na Haruni, ndivyo walivyofanya.
Ndivyo walivyofanya wana wa Israeli wote; kama BWANA alivyowaagiza Musa na Haruni, ndivyo walivyofanya.
mtawatoa nje wote, wanaume kwa wanawake, mtawaweka nje ya kambi; ili wasizitie unajisi kambi zao, ambazo mimi naketi katikati yazo.