Ndipo BWANA akamwambia Musa, Shuka chini, uwaonye watu wasije wakafanya njia kuja kwa BWANA kutazama, kisha wengi miongoni mwao wakaangamia.
Hesabu 4:20 - Swahili Revised Union Version lakini wasiingie wao kupaona mahali pale patakatifu, hata kwa dakika moja, ili wasife. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Lakini wazawa wa Kohathi hawataingia kamwe kuvitazama vitu hivyo vitakatifu sana; wakifanya hivyo watakufa.” Biblia Habari Njema - BHND Lakini wazawa wa Kohathi hawataingia kamwe kuvitazama vitu hivyo vitakatifu sana; wakifanya hivyo watakufa.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Lakini wazawa wa Kohathi hawataingia kamwe kuvitazama vitu hivyo vitakatifu sana; wakifanya hivyo watakufa.” Neno: Bibilia Takatifu Lakini Wakohathi hawaruhusiwi kuingia ndani ili kuangalia vitu vitakatifu, hata kwa kitambo kidogo, la sivyo watakufa.” Neno: Maandiko Matakatifu Lakini Wakohathi hawaruhusiwi kuingia ndani ili kuangalia vitu vitakatifu, hata kwa kitambo kidogo, la sivyo watakufa.” BIBLIA KISWAHILI lakini wasiingie wao kupaona mahali pale patakatifu, hata kwa dakika moja, ili wasife. |
Ndipo BWANA akamwambia Musa, Shuka chini, uwaonye watu wasije wakafanya njia kuja kwa BWANA kutazama, kisha wengi miongoni mwao wakaangamia.
Kisha atatia ule uvumba juu ya moto mbele za BWANA, ili moshi wa ule uvumba ukisitiri kiti cha rehema kilicho juu ya ushuhuda, asije akafa.
Tena hapo maskani itakapokwenda mbele, Walawi wataishusha; tena hapo maskani itakaposimamishwa, Walawi wataisimamisha; na mgeni atakayekaribia atauawa.
Nao watahudumu kwa kufuata amri yako, na kuhudumu hemani pote; lakini wasikaribie vyombo vya patakatifu, wala madhabahu, wasife, wao pamoja na ninyi.
Na Haruni na wanawe watakapokwisha kupafunika mahali patakatifu, na vyombo vyote vya mahali patakatifu, hapo watakapong'oa kambi; baadaye, wana wa Kohathi watakuja kuvichukua; lakini wasiviguse vile vitu vitakatifu, wasife. Vyombo vile ni mzigo wa wana wa Kohathi katika hema ya kukutania.
lakini wafanyieni neno hili, ili kwamba wawe hai, wasife, hapo watakapovikaribia vile vitu vilivyo vitakatifu sana; Haruni na wanawe wataingia ndani, na kuwawekea kila mtu utumishi wake, na kila mtu mzigo wake;
Kisha hekalu la Mungu lililoko mbinguni likafunguliwa, na sanduku la Agano lake likaonekana ndani ya hekalu lake. Kukawa na umeme, na sauti, na radi, na tetemeko la nchi, na mvua kubwa ya mawe.
Basi BWANA aliwapiga baadhi ya watu wa Beth-shemeshi, kwa sababu wamechungulia ndani ya hilo sanduku la BWANA, wapata watu sabini, na watu elfu hamsini; nao watu wakalalamika, kwa kuwa BWANA amewapiga watu kwa uuaji mkuu.