BWANA akamwambia Musa, Andika habari hii katika kitabu iwe ukumbusho, kisha ihubiri masikioni mwa Yoshua; ya kuwa nitaufuta ukumbusho wa Amaleki kabisa, usiwe tena chini ya mbingu.
Hesabu 33:2 - Swahili Revised Union Version Musa akaandika jinsi walivyotoka katika vituo, kituo baada ya kituo kwa kufuata amri ya BWANA; na hivi ndivyo vituo: Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mose aliandika jina la kila mahali walipopiga kambi, kituo baada ya kituo, kwa agizo la Mwenyezi-Mungu. Biblia Habari Njema - BHND Mose aliandika jina la kila mahali walipopiga kambi, kituo baada ya kituo, kwa agizo la Mwenyezi-Mungu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mose aliandika jina la kila mahali walipopiga kambi, kituo baada ya kituo, kwa agizo la Mwenyezi-Mungu. Neno: Bibilia Takatifu Kwa agizo la Mwenyezi Mungu, Musa aliweka kumbukumbu ya vituo katika safari yao. Hivi ndivyo vituo katika safari yao: Neno: Maandiko Matakatifu Kwa agizo la bwana, Musa aliweka kumbukumbu ya vituo katika safari yao. Hivi ndivyo vituo katika safari yao: BIBLIA KISWAHILI Musa akaandika jinsi walivyotoka katika vituo, kituo baada ya kituo kwa kufuata amri ya BWANA; na hivi ndivyo vituo: |
BWANA akamwambia Musa, Andika habari hii katika kitabu iwe ukumbusho, kisha ihubiri masikioni mwa Yoshua; ya kuwa nitaufuta ukumbusho wa Amaleki kabisa, usiwe tena chini ya mbingu.
Hivi ndivyo vituo vya wana wa Israeli, hapo walipotoka nchi ya Misri kwa vikosi chini ya uongozi wa Musa na Haruni.
Wakasafiri kutoka Ramesesi mwezi wa kwanza, siku ya kumi na tano ya mwezi wa kwanza; siku ya pili baada ya Pasaka, wana wa Israeli wakatoka kwa uhodari mkubwa mbele ya macho ya Wamisri wote,
Ni mwendo wa siku kumi na moja kutoka Horebu kwa njia ya mlima wa Seiri mpaka Kadesh-barnea.
BWANA akaniambia, Ondoka, uendelee na safari yako ukiwaongoza watu; nao wataingia waimiliki nchi, niliyowaapia baba zao ya kuwa nitawapa.