Hesabu 3:30 - Swahili Revised Union Version Na mkuu wa nyumba ya baba za jamaa za Wakohathi atakuwa Elisafani mwana wa Uzieli. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema naye Elisafani, akiwa mkuu wa ukoo huo wa familia za Wakohathi. Biblia Habari Njema - BHND naye Elisafani, akiwa mkuu wa ukoo huo wa familia za Wakohathi. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza naye Elisafani, akiwa mkuu wa ukoo huo wa familia za Wakohathi. Neno: Bibilia Takatifu Kiongozi wa jamaa za koo za Wakohathi alikuwa Elisafani mwana wa Uzieli. Neno: Maandiko Matakatifu Kiongozi wa jamaa za koo za Wakohathi alikuwa Elisafani mwana wa Uzieli. BIBLIA KISWAHILI Na mkuu wa nyumba ya baba za jamaa za Wakohathi atakuwa Elisafani mwana wa Uzieli. |
Musa akawaita Mishaeli na Elisafani, wana wa Uzieli mjombaye Haruni, na kuwaambia, Njoni karibu, mwachukue hawa ndugu zenu, mkawaondoe hapa mbele ya maskani, mwende nao nje ya kambi.
Na katika Kohathi ni jamaa ya Waamrami, na jamaa ya Waishari, na jamaa ya Wahebroni, na jamaa ya hao Wauzieli; hizo ni jamaa za Wakohathi.
Na vitu watakavyovitunza ni hilo sanduku, na meza, na kinara cha taa, na madhabahu, na vile vyombo vya mahali patakatifu wavitumiavyo katika huduma yao, na pazia, na utumishi wake wote.
Na Haruni na wanawe watakapokwisha kupafunika mahali patakatifu, na vyombo vyote vya mahali patakatifu, hapo watakapong'oa kambi; baadaye, wana wa Kohathi watakuja kuvichukua; lakini wasiviguse vile vitu vitakatifu, wasife. Vyombo vile ni mzigo wa wana wa Kohathi katika hema ya kukutania.
Huu ndio utumishi wa wana wa Kohathi katika hema ya kukutania, katika vile vyombo vitakatifu sana;