Hesabu 23:22 - Swahili Revised Union Version Mungu amewaleta kutoka Misri, Naye ana nguvu kama nguvu za nyati. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mungu aliyewachukua kutoka Misri, huwapigania kwa nguvu kama za nyati. Biblia Habari Njema - BHND Mungu aliyewachukua kutoka Misri, huwapigania kwa nguvu kama za nyati. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mungu aliyewachukua kutoka Misri, huwapigania kwa nguvu kama za nyati. Neno: Bibilia Takatifu Mungu aliwatoa kutoka Misri; wao wana nguvu kama za nyati. Neno: Maandiko Matakatifu Mungu aliwatoa kutoka Misri; wao wana nguvu za nyati. BIBLIA KISWAHILI Mungu amewaleta kutoka Misri, Naye ana nguvu kama nguvu za nyati. |
Mungu ni mwenye kutisha Kutoka patakatifu pako. Ndiye Mungu wa Israeli; Yeye huwapa watu wake nguvu na uwezo. Na ahimidiwe Mungu.
Ilikuwa mwisho wa miaka hiyo mia nne na thelathini, ilikuwa siku ile ile, majeshi yote ya BWANA yalitoka nchi ya Misri.
Ilikuwa siku ile ile moja, BWANA akawatoa wana wa Israeli katika nchi ya Misri kwa majeshi yao.
Na Wamisri watajua ya kuwa mimi ndimi BWANA, nitakapokwisha kujipatia utukufu kwa Farao, na magari yake, na farasi wake.
lakini, nilikusimamisha wewe kwa sababu ii hii, ili nikuoneshe uweza wangu, tena kwamba jina langu litangazwe katika dunia yote.
Na nyati watateremka pamoja nao, na ndama pamoja na mafahali, na nchi yao italewa kwa damu, na mavumbi yake yatanoneshwa kwa shahamu.
Basi akatuma wajumbe kwa Balaamu mwana wa Beori, hadi Pethori, ulio kando ya Mto, mpaka nchi ya wana wa watu wake, kwenda kumwita, akisema, Tazama, kuna watu waliotoka Misri; tazama, wanaufunika uso wa nchi, tena wanakaa kunikabili mimi.
Mungu amemleta kutoka Misri, Ana nguvu mfano wa nguvu za nyati; Atawameza mataifa walio adui zake, Ataivunja mifupa yao vipande vipande. Atawachoma kwa mishale yake.
Mzaliwa wa kwanza wa ng'ombe wake mume, enzi ni yake; Na pembe zake ni pembe za nyati; Kwa hizo atayasukuma mataifa yote, hata ncha za nchi; Nao ni makumi ya maelfu ya Efraimu, Nao ni maelfu ya Manase.
Maana tumesikia jinsi BWANA alivyoyakausha maji ya Bahari ya Shamu mbele yenu, hapo mlipotoka Misri, tena mambo hayo mliyowatendea wafalme wawili wa Waamori waliokuwa huko ng'ambo ya Yordani, yaani, Sihoni na Ogu, mliowaangamiza kabisa.