Ndipo akaondoka Eliashibu, kuhani mkuu, pamoja na nduguze makuhani, wakalijenga lango la kondoo; wakazitia boriti zake, wakaisimamisha milango yake; mpaka mnara wa Hamea wakalitakasa, mpaka mnara wa Hananeli.
Hesabu 21:18 - Swahili Revised Union Version Kisima walichokichimba wakuu, Ambacho wakuu wa watu wakakifukua, Kwa fimbo za enzi, kwa fimbo zao. Kutoka lile jangwa wakaenda Matana; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kisima kilichochimbwa na wakuu kilichochimbwa sana na wenye cheo, kwa fimbo zao za enzi na bakora.” Kutoka jangwani walisafiri mpaka Matana, Biblia Habari Njema - BHND Kisima kilichochimbwa na wakuu kilichochimbwa sana na wenye cheo, kwa fimbo zao za enzi na bakora.” Kutoka jangwani walisafiri mpaka Matana, Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kisima kilichochimbwa na wakuu kilichochimbwa sana na wenye cheo, kwa fimbo zao za enzi na bakora.” Kutoka jangwani walisafiri mpaka Matana, Neno: Bibilia Takatifu kuhusu kisima ambacho kilichimbwa na wakuu, ambacho watu mashuhuri walikifukua, watu mashuhuri wakiwa na fimbo za utawala na bakora.” Kisha wakatoka jangwani kwenda Matana, Neno: Maandiko Matakatifu kuhusu kisima ambacho kilichimbwa na wakuu, ambacho watu mashuhuri walikifukua, watu mashuhuri wakiwa na fimbo za utawala na bakora.” Kisha wakatoka jangwani kwenda Matana, BIBLIA KISWAHILI Kisima walichokichimba wakuu, Ambacho wakuu wa watu wakakifukua, Kwa fimbo za enzi, kwa fimbo zao. Kutoka lile jangwa wakaenda Matana; |
Ndipo akaondoka Eliashibu, kuhani mkuu, pamoja na nduguze makuhani, wakalijenga lango la kondoo; wakazitia boriti zake, wakaisimamisha milango yake; mpaka mnara wa Hamea wakalitakasa, mpaka mnara wa Hananeli.
Na baada yao wakajenga Watekoi; lakini wakuu wao hawakutia shingo zao kazini mwa bwana wao.
Kwa maana BWANA ndiye mwamuzi wetu; BWANA ndiye mfanya sheria wetu; BWANA ndiye mfalme wetu; ndiye atakayetuokoa.
Kwa kuwa torati ilitolewa kwa mkono wa Musa; neema na kweli zilikuja kwa mkono wa Yesu Kristo.
Lakini wewe, simama hapa karibu nami, nami nitasema nawe sheria zote, na amri na hukumu, utakazowafunza, wapate kuzifanya katika nchi niwapayo kuimiliki.
Mtoa sheria na mwenye kuhukumu ni mmoja tu, ndiye awezaye kuokoa na kuangamiza. U nani wewe umhukumuye mtu mwingine?