Kisha beramu ya kambi ya Reubeni ikasafiri kwenda mbele kwa majeshi yao; na juu ya jeshi lake alikuwa Elisuri mwana wa Shedeuri.
Hesabu 2:16 - Swahili Revised Union Version Wote waliohesabiwa katika kambi za Reubeni walikuwa elfu mia moja hamsini na moja na mia nne na hamsini, kwa majeshi yao. Nao ndio watakaofuata wakiwa kundi la pili. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Jumla ya wanaume watakaokuwa katika kambi ya Reubeni kulingana na makundi yao ni watu 151,450. Hawa ndio watakaokuwa katika msafara wa pili. Biblia Habari Njema - BHND Jumla ya wanaume watakaokuwa katika kambi ya Reubeni kulingana na makundi yao ni watu 151,450. Hawa ndio watakaokuwa katika msafara wa pili. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Jumla ya wanaume watakaokuwa katika kambi ya Reubeni kulingana na makundi yao ni watu 151,450. Hawa ndio watakaokuwa katika msafara wa pili. Neno: Bibilia Takatifu Wanaume wote walio katika kambi ya Reubeni, kufuatana na makundi yao, ni elfu mia moja hamsini na moja na mia nne na hamsini (151,450). Nao watakuwa nafasi ya pili kuondoka. Neno: Maandiko Matakatifu Wanaume wote walio katika kambi ya Reubeni, kufuatana na makundi yao, ni 151,450. Nao watakuwa nafasi ya pili kuondoka. BIBLIA KISWAHILI Wote waliohesabiwa katika kambi za Reubeni walikuwa elfu mia moja hamsini na moja na mia nne na hamsini, kwa majeshi yao. Nao ndio watakaofuata wakiwa kundi la pili. |
Kisha beramu ya kambi ya Reubeni ikasafiri kwenda mbele kwa majeshi yao; na juu ya jeshi lake alikuwa Elisuri mwana wa Shedeuri.
na jeshi lake, na wale waliohesabiwa kwao, walikuwa elfu arubaini na tano, mia sita na hamsini.
Wote waliohesabiwa katika kambi ya Efraimu walikuwa elfu mia moja na nane na mia moja, kwa majeshi yao. Nao ndio watakaoondoka wakiwa kundi la tatu.
Wote waliohesabiwa katika kambi ya Dani walikuwa elfu mia moja hamsini na saba na mia sita. Hao ndio watakaoondoka mwisho kwa kufuata bendera yao.
Hao wote waliohesabiwa katika kambi ya Yuda walikuwa elfu mia moja themanini na sita na mia nne, kwa makundi yao. Hao ndio watakaotangulia mbele.