Tena ikawa, walipokuwa wakiwaua, nami nikaachwa, nilianguka kifudifudi, nikalia, nikasema, Ee Bwana MUNGU! Utaangamiza mabaki yote ya Israeli, wakati wa kumwaga ghadhabu yako juu ya Yerusalemu?
Hesabu 16:4 - Swahili Revised Union Version Musa aliposikia maneno haya, akaanguka kifudifudi; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mose aliposikia hayo, alijitupa chini kifudifudi. Biblia Habari Njema - BHND Mose aliposikia hayo, alijitupa chini kifudifudi. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mose aliposikia hayo, alijitupa chini kifudifudi. Neno: Bibilia Takatifu Musa aliposikia jambo hili, akaanguka kifudifudi. Neno: Maandiko Matakatifu Musa aliposikia jambo hili, akaanguka kifudifudi. BIBLIA KISWAHILI Musa aliposikia maneno haya, akaanguka kifudifudi; |
Tena ikawa, walipokuwa wakiwaua, nami nikaachwa, nilianguka kifudifudi, nikalia, nikasema, Ee Bwana MUNGU! Utaangamiza mabaki yote ya Israeli, wakati wa kumwaga ghadhabu yako juu ya Yerusalemu?
Nao wakaanguka kifudifudi, wakasema, Ee Mungu, Mungu wa roho za wenye mwili wote, je! Mtu mmoja atafanya dhambi, nawe utaukasirikia mkutano wote?
kisha akanena na Kora na mkutano wake wote, akawaambia, Asubuhi BWANA ataonesha ni kina nani walio wake, kisha ni nani aliye mtakatifu, tena ni nani atakayemkaribisha kwake; maana, yeye atakayemchagua ndiye atakayemsongeza kwake.
Musa na Haruni wakatoka pale palipokuwa mkutano, wakaenda hadi mlangoni pa hema ya kukutania, wakaanguka kifudifudi; utukufu wa BWANA ukawatokea.
Yoshua akararua mavazi yake, akaanguka kifudifudi mbele ya sanduku la BWANA hadi jioni, yeye na wazee wa Israeli; wakatia mavumbi vichwani mwao.