Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yoshua 7:6 - Swahili Revised Union Version

6 Yoshua akararua mavazi yake, akaanguka kifudifudi mbele ya sanduku la BWANA hadi jioni, yeye na wazee wa Israeli; wakatia mavumbi vichwani mwao.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

6 Yoshua akayararua mavazi yake, yeye pamoja na wazee wa Israeli. Wakajitupa chini mbele ya sanduku la Mwenyezi-Mungu mpaka jioni; wakajitia mavumbi vichwani mwao.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

6 Yoshua akayararua mavazi yake, yeye pamoja na wazee wa Israeli. Wakajitupa chini mbele ya sanduku la Mwenyezi-Mungu mpaka jioni; wakajitia mavumbi vichwani mwao.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

6 Yoshua akayararua mavazi yake, yeye pamoja na wazee wa Israeli. Wakajitupa chini mbele ya sanduku la Mwenyezi-Mungu mpaka jioni; wakajitia mavumbi vichwani mwao.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

6 Ndipo Yoshua akayararua mavazi yake, akaanguka kifudifudi mbele ya Sanduku la Mwenyezi Mungu, na akabakia hapo hadi jioni. Wazee wa Israeli nao wakafanya vivyo hivyo, wakatia mavumbi vichwani mwao.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

6 Ndipo Yoshua akayararua mavazi yake, akaanguka kifudifudi mbele ya Sanduku la bwana, na akabakia hapo mpaka jioni. Wazee wa Israeli nao wakafanya vivyo hivyo wakatia mavumbi vichwani mwao.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

6 Yoshua akayararua mavazi yake, akaanguka kifudifudi mbele ya sanduku la BWANA hadi jioni, yeye na wazee wa Israeli; wakatia mavumbi vichwani mwao.

Tazama sura Nakili




Yoshua 7:6
30 Marejeleo ya Msalaba  

Akarudi Reubeni birikani, kumbe! Yusufu hayumo katika birika, akararua nguo zake.


Yakobo akararua mavazi yake, akajivika gunia viunoni, na kumlilia mwanawe siku nyingi.


Ndipo Daudi akashika nguo zake akazirarua na kadhalika watu wote waliokuwa pamoja naye;


wakaomboleza, wakalia, wakafunga hadi jioni, kwa ajili ya Sauli, na kwa ajili ya Yonathani mwanawe, na kwa ajili ya watu wa BWANA na kwa ajili ya nyumba ya Israeli; kwa sababu wameanguka kwa upanga.


hata siku ya tatu ikawa, tazama! Akaja mtu kutoka kambi ya Sauli, nguo zake zimeraruliwa, tena ana mavumbi kichwani mwake; basi, ikawa alipomfikia Daudi, akaanguka chini, akamsujudia.


Basi Daudi akamwomba Mungu kwa ajili ya mtoto; Daudi akafunga, akaingia, akalala chini usiku kucha.


Naye Tamari akatia majivu kichwani mwake, akairarua hiyo kanzu ndefu yake aliyoivaa, akaweka mkono kichwani akaenda zake huku akilia kwa sauti.


Ndipo mfalme akainuka, akararua nguo zake, akalala chini; nao watumishi wake wote wakasimama karibu naye, nguo zao zikiwa zimeraruliwa.


Ikawa, mfalme alipokwisha kuyasikia maneno ya kitabu hicho cha torati, alirarua nguo zake.


Ikawa, mfalme alipoyasikia maneno ya torati, aliyararua mavazi yake.


Basi hapo Ezra alipokuwa akiomba na kuungama, akilia, na kujiangusha kifudifudi mbele ya nyumba ya Mungu, kusanyiko kubwa sana la wanaume, wanawake na watoto, kutoka katika Israeli likamkusanyikia; maana watu hao walikuwa wakilia sana.


Hata siku ya ishirini na nne ya mwezi huo wana wa Israeli wakawa wamekusanyika, wakifunga, wenye kuvaa magunia, na kujitia udongo vichwani.


Basi Mordekai alipojua mambo yote yaliyofanyika, alizirarua nguo zake, akajivika gunia na kujipaka majivu, akatoka hadi katikati ya mji, akalia kwa sauti kuu ya uchungu.


Na katika kila mkoa, ambako amri ya mfalme na mbiu yake imewasili, palikuwako msiba mkuu kwa Wayahudi, na kufunga, na kulia, na kuomboleza; hata na wengi wakalala juu ya gunia na majivu.


Ndipo Ayubu akainuka, akalirarua joho lake, kisha akanyoa kichwa chake, na kuanguka chini, na kusujudia;


Basi walipoinua macho yao, wakiwa bado kwa mbali, wasimtambue, wakainua sauti zao na kulia; kila mmoja akararua joho lake, wakarusha mavumbi juu ya vichwa vyao kuelekea mbinguni.


Kwa sababu hiyo najichukia nafsi yangu, na kutubu Katika mavumbi na majivu.


Wazee wa binti Sayuni huketi chini, Hunyamaza kimya; Wametupa mavumbi juu ya vichwa vyao, Wamejivika viunoni nguo za magunia; Wanawali wa Yerusalemu huinama vichwa vyao Kuielekea nchi.


Na Yoshua mwana wa Nuni, na Kalebu mwana wa Yefune, waliokuwa miongoni mwao walioipeleleza nchi, wakararua nguo zao;


Nao wakaanguka kifudifudi, wakasema, Ee Mungu, Mungu wa roho za wenye mwili wote, je! Mtu mmoja atafanya dhambi, nawe utaukasirikia mkutano wote?


Ondokeni kati ya mkutano, ili niwaangamize mara moja. Wao wakaanguka kifudifudi.


Lakini mitume Barnaba na Paulo, walipopata habari, wakararua nguo zao, wakaenda mbio wakaingia katika umati wa watu, wakipiga kelele,


Yoshua akasema, Ee Bwana MUNGU, kwa nini umewavusha watu hawa mto wa Yordani, ili kututia katika mikono ya Waamori, na kutuangamiza? Laiti tu, tungaliridhika kukaa ng'ambo ya Yordani


Wakatupa mavumbi juu ya vichwa vyao, wakalia, wakitokwa na machozi na kuomboleza, wakisema, Ole, ole, mji ule ulio mkuu! Ambao ndani yake wote wenye merikebu baharini walipata mali kwa utajiri wake; kwa kuwa katika saa moja umekuwa ukiwa.


Ikawa alipomuona akayararua mavazi yake, akasema, Ole wangu! Mwanangu, umenitweza sana, nawe u mmoja miongoni mwa hao wanisumbuao; kwa kuwa mimi nimemfunulia BWANA kinywa changu, nami siwezi kurudi nyuma.


Wana wa Israeli wakakwea juu na kulia mbele za BWANA hadi jioni; wakamwuliza BWANA, wakisema, Je! Niende nikaribie tena kupiga vita juu ya wana wa Benyamini ndugu yangu? BWANA akasema, Haya, kweeni, mwende kupigana naye.


Ndipo wana wa Israeli wote, na hao watu wote, wakakwea, wakaenda Betheli, na kulia, wakaketi hapo mbele za BWANA, wakafunga siku hiyo hadi jioni; nao wakasongeza sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani mbele za BWANA.


Basi hao watu wakafika Betheli, wakaketi huko mbele ya Mungu hadi jioni, nao wakainua sauti zao na kulia sana.


Basi, mtu mmoja wa Benyamini akapiga mbio kutoka mle vitani akafika Shilo siku ile ile, hali nguo zake zimeraruliwa, na mavumbi kichwani mwake.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo