Hivyo BWANA aliposikia akaghadhibika; Moto ukawashwa juu ya Yakobo, Hasira nayo ikapanda juu ya Israeli.
Hesabu 11:3 - Swahili Revised Union Version Jina la mahali hapo likaitwa Tabera kwa sababu huo moto wa BWANA ukawaka kati yao. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kwa hiyo, mahali hapo pakaitwa Tabera, kwa sababu hapo moto wa Mwenyezi-Mungu uliwaka kati ya watu. Biblia Habari Njema - BHND Kwa hiyo, mahali hapo pakaitwa Tabera, kwa sababu hapo moto wa Mwenyezi-Mungu uliwaka kati ya watu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kwa hiyo, mahali hapo pakaitwa Tabera, kwa sababu hapo moto wa Mwenyezi-Mungu uliwaka kati ya watu. Neno: Bibilia Takatifu Hivyo mahali pale pakaitwa Tabera, kwa sababu moto kutoka kwa Mwenyezi Mungu uliwaka miongoni mwao. Neno: Maandiko Matakatifu Hivyo mahali pale pakaitwa Tabera, kwa sababu moto kutoka kwa bwana uliwaka miongoni mwao. BIBLIA KISWAHILI Jina la mahali hapo likaitwa Tabera kwa sababu huo moto wa BWANA uliwaka kati yao. |
Hivyo BWANA aliposikia akaghadhibika; Moto ukawashwa juu ya Yakobo, Hasira nayo ikapanda juu ya Israeli.
Kisha mkutano wa wafuasi waliokuwa kati yao, wakashikwa na tamaa; wana wa Israeli nao wakalia tena, wakasema, Ni nani atakayetupa nyama tule?
Kisha moto ukatoka kwa BWANA, ukawateketeza hao watu mia mbili hamsini waliofukiza uvumba.